Sunday, January 20, 2013

CUF wakana tuhuma za ufisadi

Written by  Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akifafanua jambo

           Tanga

WAKATI vyama vya siasa vikiendelea na propaganda za siasa za kifisadi na majungu, huku pia vikitupia lawama Chama Cha Mapindunzi (CCM) kwa Ufisadi Chama cha Wananchi CUF kimekana tuhuma za ufisadi wa kumiliki migodi minane ya madini Mkoani Tanga.

Akizungumza na Habarimpya.com Katibu wa CUF Wilaya ya Handeni, Masoud Mjaila alikiri kuwa CUF inamiliki Kampuni ya uchimbaji wa madini katika  Kijiji cha Sezakofi, Kata ya Ndolwa.

Alisema CUF inamiliki Kampuni hiyo na kwamba migodi hiyo ya madini pia wanaimiliki kihalali huku akionyesha vibali, hatua iliyolenga kujaribu kujisafisha, kufuatia kurushiwa tuhuma na Mlezi wa ADC Kanda ya Kaskazini, Hassan Doyo, aliyejiunga na chama hicho baada ya kutimuliwa CUF.

“Wananchi msikubali kuburuzwa, hiki chama chenu cha CUF kina miaka 20 tangu kuanzishwa, hapa Handeni kina miaka 15, lakini mnaona hali ilivyo, ndiyo hivi karibuni sasa na sisi tupo ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Mjaila na kuongeza:

“Sasa hawa ADC wameanza jana, leo wanataka waungwe mkono, hapana! Hawa wanatafuta masilahi yao maana huku CUF walifukuzwa, eti wanasema migodi ile ya madini haina vibali, siyo kweli kwani serikali iko wapi, tumechangia zaidi ya Sh3.5 milioni, kusaidia miradi mbalimbali ya Serikali ya Kijiji cha Sezakofi.”

Alisema wanatambua vijembe hivyo vinatokana na fitina zilizojaa viongozi wa ADC, hawataki CUF wapate maendeleo. Aliwashauri nao kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya kujipatia maendeleo badala ya malumbano majukwaani.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger