Thursday, June 27, 2013

CCM YAVUNA WANACHAMA WAPYA JIMBO LA MCHINGA - LINDI

image description

WANACHAMA wa chama cha mapinduzi Kata ya mipingo Kijiji cha Matapwa wilaya Lindi Jimbo la mchinga wakicheza kwa furaha baada kuwapokea wanachama zaidi ya 120 waliohama chama cha wananchi CUF na kujiunga na CHAMA CHA MAPINDUZI tukio limesababisha tawi la chama cha wananchi kubaki na mwenyekiti na katibu wake.

image description

Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Alli Mtopa akimkabidhi kadi ya CCM miongoni mwa wanachama 120 wa kijiji cha Matapwa jimbo la mchinga hadija Saidi aliyehama chama cha wananchi CUF na kujiunga na CHAMA CHA MAPINDUZI .

image description

Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Alli Mohamed Mtopa akimkabidhi kadi ya CCM Fatuma hamisi mkazi wa kijiji cha Matapwa jimbo la mchinga aliyeyehama chama cha wananchi CUF na kujiunga na CHAMA CHA MAPINDUZI.

image description

WANACHAMA wa chama cha mapinduzi Kata ya mipingo Kijiji cha Matapwa wilaya Lindi Jimbo la mchinga wakicheza kwa furaha baada kuwapokea wanachama zaidi ya 120 waliohama chama cha wananchi CUF na kujiunga na CHAMA CHA MAPINDUZI tukio limesababisha tawi la chama cha wananchi kubaki na Mwenyekiti na Katibu wake.

image description
Na Abdulaziz video -MICHUZI BLOG

WANACHAMA wa chama cha wananchi (CUF ) Tawi la Matapwa Jimbo la Mchinga wamekiama chama hicho na kuamia chama cha mapinduzi huku wakiliacha tawi ili likibaki na wanachama wawili akiwemo Mwenyekiti na Katibu yake.

Tukio hilo limetokea jana kwenye mkutano wa adhara uliitishwa na Mbunge wa jimbo la Mchinga Saidi Mtanda wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo hilo.

Akizungumza kabla ya kugawa kadi kwa wanachama zaidi ya 120 wa tawi hilo lililokuwa ngome ya CUF katika jimbo Hilo la Mchinga kiongozi mwandamizi wa CHAMA MCHA MAPINDUZI Taifa Tambwe Hiza aliwataka wananchi wa kata hiyo kuachana na siasa za kichochezi zinazo sababisha uvunjifu wa amani badala yake wafanye kazi za kujiletea maendeleo yao.

Tambwe alisema hakuna chama kinachotawala duniani ambacho kinagawa fedha kwa wananchi wake kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku bali ilani, na sera mzuri kama za ccm ndizo zinawafanya wananchi wao kuwa na maendeleo ikiwemo upataji wa huduma muhimu za kijamii kama vile. Maji, elimu, miundombinu pamoja na huduma za Afya.

Aidha Tambwe aliwaomba wanananchi wa jimbo hilo ambao hawajajiunga na chama hicho kujiunga haraka na kuachana vyama vyenye itikadi za kibaguzi, kidini na kueleza kuwa CHAMA CHA MAPINDUZI ndicho chama pekee nchini chenye sera mzuri na mwelekeo wa kuwaletea maendeleo wananchi yake.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger