Thursday, January 31, 2013

KINANA WEE ACHA TU, ASHIRIKI KIKWELI UJENZI WA MIRADIDUNDO UJENZI WA MIRADI KIBONDO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo amedhihirisha kuwa ni mtu wa vitendo zadi kuliko maneno, baada ya kuonyesha uwezo wake wa kufanya kazi za kijamii kwa umahiri mkubwa, kwa kushiriki katika ujenzi wa chumba cha darasa katika shule ya Sekondari Kumwambo   na ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Bunyambo, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, ambayo ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma. Pichani Kinana akishiriki ujenzi wa darasa katika shule ya sekondari Kumwambo, Kibondo
 Kinana akiongoza ujenzi wa chumba cha darasa kwenye shule ya sekondari Kumwambo. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Abdallah Bulembo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Walid Kaborou
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananfunzi wa shule hiyo baada ya kushiriki ujenzi huo. Baadaye Kinana alienda na msafara wake Kijiji cha Bunyambo ambako pia alishiriki ujenzi wa Ofisi ya tawi la CCM na kuahidi kuwapa sh. milioni 2 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi.
 Kinana akiongoza ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Bunyambo, wilayani Kibondo mkoani Kigoma
Kinana akihakiki kwa kipimo wakati akiendelea na ujenzi kwenye ofisi hiyo ya CCM. Kulia ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Kigoma, Stanley Mkandawile
 Kinana akitazama kama tofali limekaa sawa, wakati akishiriki kujenga Ofisi hiyo ya CCM
 LETE TOFALI: Anasema Kinana kumwambia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Kaborou wakati akiendelea kushiriki ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM

 Kisha Kinana akawaaga wananchi waliohudhuria kwenye Ujenzi wa Ofisi hiyo

Katibu Mkuu wa CCM (kushoto) na ujumbe wake wakichagua miwa kwa muuzaji waliyemkuta njiani wakati wakitemebea kwa mguu kiasi cha kilometa moja na nusu kwenda kwenye mkutano wa hadhara baada ya ujenzi huo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger