Monday, January 28, 2013

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI ATOA MAONI YA KATIBA MPYA KWA TUME

  Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Hassan Mwinyi (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya katiba, walioongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Ndg Joseph Warioba (kulia). 
Wajumbe wa Tume walikutana na huyo Rais mstaafu ili kupata maoni na uzoefu wake 
katika uandishi wa Katiba mpya.
 Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya zanzibar, Ndg. Othman Masoud Othman (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Tume hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume . 
Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo , Jaji Joseph warioba.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Hassan Mwinyi (kushoto) akibadilishana mawazo na
 Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt.Salim Ahmed Salim (kulia) na 
Makamu Mwenyekiti, Jaji Mkuu  mstaafu, Augustino Ramadhani (katikati).Wajumbe wa Tume walikutana na huyo Rais mstaafu ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba mpya.
Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serekali ya Tanzania, Andrew Chenge akizungumza na Wajumbe  wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Mkutano baina yao uliofanyika katika Ofisi za Tume hiyo 
Jijini Dar es Salaam kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume. 
Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume,Jaji Mkuu Mstaafu Ramadhani.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger