Monday, February 11, 2013

KIKAO CHA NEC YA CCM,MJINI DODOMA LEO

Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa kuendelea na semina, leo kwenye Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na
 Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa semina iliyoanza jana, na kuendelea leo kwenye ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Pamoja naye ni Dk. Sheni na Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji, kabla ya kuanza kikao hicho leo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisahuriana jambo ukumbini na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, kabla ya kikao kuanza leo
Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akimsalimia Katibu wa NEC Siasa ana Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kabla ya kikao kuanza ukumbini. Katikati ni Katibu wa NEC, 
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Hali ndani ya ukumbi ilikuwa kama hivi kabla ya kikao kuanza. Kushoto Kabisa ni Nape na 
Zakia Meghji na juu-kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wajumbe. 
Na Kulia chini ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhamed Seif Khatib na
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakiteta jambo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Vuai Ali Vuai kabla ya kikao kuanza
Wajumbe wa NEC  Profesa Anna Tibaijuka na Mzee Mtandika wakibadilishana mawazo ukumbini
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akichati jambona Mjumbe wa NEC, Samwel Sitta na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kikao
Nape (kulia) akichangia kwenye mazungumzo hayo kati yake na Dk. Asha-Rose na Sitta
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC, William Mukama akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzake wa NEC Profesa Juma Kapuya ukumbini
Hii ndiyo Sekretarieti inayofuatilia na kuweka kumbukumbu ya mijadala inayozungumzwa kwenye mkutano huo
HII UNAONAJE?  Mjumbe wa NEC, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe akiteta jambo na 
Mzee Mtandika
Katibu Mkuu wa UWT, Sophia Simba akijadiliana jambo wa Wajumbe wenzake wa NEC ukumbini. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo Ana Makilagi.
Dk. Asha-Rose Migiro akishauriana jambo na Nape
TUKIFANYA HIVI MAMBO YATANYOOKA AU SIYO? Inaelekea ndivyo Dk. Asha-Rose Migiro alivyokuwa akisema kumwambia Nape katika mazungumzo yao ukumbi kabla ya kikao
HAPO VIPI? Katibu wa Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib anaonekana kumuuliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati wakibadilishana mawazo kabla ya kikao kuanza
SALAMU! Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa, Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia wajumbe wenzake wa NEC ukumbini kabla ya kikao kuanza
Wajumbe wakisubiri kwa hamu kikao kuanza
Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal (kulia) na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa safu ya mbele na baadhi ya wajumbe kwenye kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wakipitia nyaraka muhimu kabla ya kikao kuanza
 
Aliyekuwa Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma aka Mama Mshua (kulia) akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabiba nje ya ukumbi. Katikati ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba
ENZI ZETU ZA IGUNGA VIPI? Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba anaonekana kumuuliza swali hilo Mjumbe wa NEC, aliyekuwa mbunge wa Igunga  Dk. Dalaly Kafumu walipokutana nje ya ukumbi kabla ya kikao kuanza
SHIKAMOO BOSI WANGU WA ZAMANI! Kaim Katibu wa CCM wa mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda akiwa na Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, William Mukama nje ya Ukumbi. Sixtus amewahi kuwa Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi kabla ya kuhamishiwa Morogoro mwaka jana wakati Mukama akiwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa.
CCM MAMBO SAFI TU! Mukama akimwambia Mjumbe wa NEC, Steven Wasira nje ya ukumbi
Wajumbe wa NEC wakiangua kicheko cha kutaniana kaba la kuingia ukumbini. Kutoka kulia ni Dk. Rafael Chegeni, Januari Makamba, Halimenshi Mayonga na Samwel Sitta
Wajumbe wakiwa tayari kuingia ukumbini kuanza kikao leo. 
 


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa akibadilishana mawazo na Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudencia Kabaka wakati wa Mkutano wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ambapo leo semina juu ya Mikakati ya Kuondoa tatizo la ajira nchini.
 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Ndugu Mwigulu Nchemba  akijadiliana jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa wakati wa semina juu ya kuondoa tatizo la ajira nchi.
 Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi na Katibu wa NEC,Uchumi na Fedha wakijadili jambo la ajira kwa nchi nzima wakati wa semina ya mikakati ya kuondoa tatizo la ajira nchini, leo kwenye ukumbi wa NEC,Dodoma.



Wajumbe wakiwa kwenye semina ya Mikakati ya Kuondoa tatizo la ajira nchini.
 
 Ally A. Msaki akitoa mada juu ya HALI YA AJIRA NCHINI NA MIKAKTI YA SERIKALI kwa niaba ya Waziri wa Kazi na Ajira,kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, inayofanyika Dodoma leo.



Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kwa makini semina juu ya Mikakati ya kuondoa tatizo la Ajira Nchini
 
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger