Thursday, March 28, 2013

HABARI KATIKA PICHA ZA RAIS KIKWETE AKIZINDUA TAARIFA YA UTAFITI WA VIASHIRIA VYA UKIMWI NA MALARIA MWAKA 2012

Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akikata ukanda kuzindua rasmi taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 - Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe William Lukuvi.



r3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa kuzindua rasmi  taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012- Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua juu baada ya taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 - Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda', Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho.
r4
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akipitia baada ya kuzindua rasmi  taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 - Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na kushoto kwake ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi, Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa
Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho akisoma taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini 
Dar es salaam.

Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiangalia matangazo ya kupiga vita UKIMWI na Malaria wakati wa uzinduzi rasmi wa taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 - Machi 27, 2013
 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU.

 by Pamela Mollel

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger