Wednesday, March 27, 2013

ZIARA YA RAIS WA CHINA XI JINPING JIJINI DAR ES SALAAM








Rais Xi Jinping akiwa ameongozana na mkewe


Rais Xi na Mkewe  wakipokelewa kwa furaha na mashada ya maua na watoto kama inavyoonekana kwenye picha.,mara baada ya kuwasili nchini.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Xi Jinping na mkewe Moscow mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam

Mapokezi ya Rais Xi Jinping katika Hoteli ya Serena Inn Jijini Dar es Salaam

Msafara wa Rais Xi Jinping ukiwasili Ikulu

Rais Dkt. Jakaya Kikwete na mgeni wake Rais Xi Jinping wakipita katikati ya umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kumpokea

Rais Dkt. Jakaya Kikwete na mgeni wake Rais Xi Jinping wakiwapungia wananchi waliojitokeza kumlaki.

Wakiwa katika mazungumzo


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa 
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Ukumbi huo umejengwa kwa ushirikiano 
kati ya Serikali ya China na Tanzania.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Xi Jinping wa China wakishangilia jambo wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wageni waliohudhuria sherehe za makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa China Mhe.Xi Jinping wakiangalia picha za matukio mbalimbali yanayohusu historia ya ushirikiano kati ya China na Tanzania katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere wakati wa sherehe za makabidhiano ya ukumbi huo jijini Dar es Salaam

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa China Mhe.Xi Jinping pamoja na Mkewe katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere muda mfupi baada ya sherehe za ufunguzi wa ukumbi huo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza hotuba ya Rais Xi Jinping aliyoitoa kuhusu Bara la Afrika.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa sherehe za makabidhiano ya
Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere



Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa China Xi Jinping wakiweka mashada ya maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA.Viongozi hao waliweka mashada hayo ya maua katika makaburi hayo yaliyopo katika kijiji cha Majohe,Ukonga jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa China Mama Peng Liyuan wakiweka maua katika makaburi ya wataalamu wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA huko katika kijiji cha Majohe,Ukonga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wa Rais Xi Jinping wakishuhudia
(picha na Freddy Maro).

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger