Friday, April 12, 2013

RAIS DK.JAKAYA M. KIKWETE AKIFUNGA SEMINA YA UTEKELEZAJI WA MFUMO MPYA WA UTENDAJI SERIKALINI KWA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkOFMBCIeBOP7AYZJHHm7Be97AaYy8CRQTPkKcQD2X9T3FkiYeYQuJeAKdKQ47nU7Q4TzsP6SEYGSTeRxJ6344DmSmK8aoB33sNx-Cmol0kPBL0iIPp7t1Rzr0HW__20o7WxQ-48IrbPFt/s1600/pe6.jpg
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akifunga semina ya Mawaziri na Makatibu Wakuu ili kupanga mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji tathmini na miradi ya maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Mfumo huo unaanza kutekelezwa kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President's Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete tarehe 22 Februari, 2013 na kukamilika Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya Kwanza wa kimaabara ( labs) yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji, miundombinu na uchukuzi.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9Kq9ddAjJnioTKqUVxu19IRJQCSGu1_NUeiJAmEo4hgowlhBWhwSyiVKZ4GvqxEAvFRW-iJaSHvnwYwD6QMiRZCag35hsBNNTTroTt9LauSTUXvTI3YpzGjlnCQOD72BFMshRW0fFD5Go/s1600/pe3.jpg
Rais Dk. Jakaya M. Kikwete, na Makamu , Rais Dk.Mohamed Gharib Bilali na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakiweka sahihi kama  wadhamini wa waraka katika utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara hizo sita katika semina elekezi kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjetf5AYbTpjIe0yJ5aTjFVeRQNvs7dvhw5Nbhs91p2bG04WwlGSPa_5TvJbIihJw8tuWxScNzRdHbl-d-HIm6rxf8vUGoUhCnv8XjlW_EcAELjZQ6NoHU6QeXXLJEveRdkTj1UfBqYkXCd/s1600/pe5.jpg

Rais Dk. Jakaya M. Kikwete akiongea wakati wa semina kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu kujadili mikakati ya utekelezaji WA WA mfumo mpya kusimamia utekelezaji, na ufuatiliaji tathmini ya miradi ya maendeleo katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimzThOiZupXer6R-ZOBWfyfZ4G-nhz7RJP3ywwfQAtY20I63IBFWHUshw5iUgCVYG1ixYOySWxfF8MkUVmmf29GIY8MIa34n7AHDR2fEYUL0nIJKfVs-ZWAKOQ80RJR4O0EkDI3Xar07tW/s1600/pe4.jpg

Mawaziri wa Fedha, Kilimo, Uchukuzi, Maji, Nishati na na Madini Elimu wakiweka saini waraka wa utekelezaji wa mfumo mpya kusimamia utekelezaji , ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara sita hizo sita baada ya semina elekezi kwa mawaziri na makatibu wakuu iliyofanyika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjw74Q7wATyh7JrkPfiA3mFg3vqdi3bvSoUUqrHlr693vv1_9BLiJaIsHYDfdyEoeB0PZ5xWo2Jiu8Sp2NlLXAGzenY1zWWEG3pKI9NqVMemaR0i5DMrOasQeA7cwGr0-h6iqlcdms68tss/s1600/pe2.jpg
Rais Dk. Jakaya M. Kikwete, na Makamu , Rais Dk.Mohamed Gharib Bilali na Katibu Mkuu Kiongozi Ndg. Ombeni Sefue wakiwa na Mawaziri na Makatibu Wakuu wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) wa Malaysia Dkt Idris Jala wakati wa kuujadili mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo uliokabidhiwa kwa wizara hizo sita katika semina elekezi kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu iliyofanyika ukumbi wa 
St Gaspar mjini Dodoma.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXaUw7Pk3y5LTwI27jnwaV1IbhBJ8t3jDcLNxtTb4MJFOxbsOaLI6b6bMQhNRiq4lXgpUAX1ABqo_Zn4Z-YWPo_0Rn5Hu5Fpcwg5Sz2DWcDLFzZqsQCP2uyVbTI4zm9JOAT6OPUyfOeY8J/s1600/pe1.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa  Benki ya Zamani ya NBC  Ndg. Lawrence Mafuru akitoa majumuisho ya uchambuzi wa kimaabara kwa kina (labs) mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji tathmini na ya ya miradi maendeleo katika semina elekezi kwa  Mawaziri na Makatibu Wakuu iliyofanyika ukumbi wa  St Gaspar mjini Dodoma. picha NA IKULU (MICHUZI)

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger