Saturday, June 15, 2013

CCM WAHITIMISHA KAMPENI ZA UCHAGUZI JIJINI ARUSHA


Juliana Shonza ambaye ni mmoja wa wanachama wa CCM wanaopigania chama kwenye kampeni za uchaguzi wa udiwani jijini Arusha.Juliana amewaomba wananchi kudumisha amani siku ya kesho kwenye zoezi la upigaji kura.Photo by Sanga Richard


"Mmemuonaaaaa?Huyu ndiye chaguo la kimadolu.CCM ndio chama cha kuwaletea maendeleo.Chuki mnazojazwa kuhusu CCM na serikali yake nizauongo kwasababu wao hawanachakuonesha walichokifanya kwaajili ya Kimadolu.Mchagueni Bi.Edna Jonathan saul mujihakikishie kata yenu kufikiwa na maendeleo ya halmashauri."  Photo by Sanga Richard

Mnapo sema CCM imejaa wazee"kwani sisi ni wazee?"Photo by Sanga Richard
Naibu katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara Mh.Mwigulu Lameck Nchemba Madelu akiwasili kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa udiwani Jijini Arusha kata ya kimadolu hii leo tar.15/06/2013.Photo by Sanga Richard
Mapokezi yamepamba moto.Photo by Sanga Richard
Huyu ni kada wa CCM anayefahamika kwa jina la Mtela Mwampamba.Amepata nafasi ya kuwa mmoja ya safu ya makada wa CCM walioongoza timu ya kampeni jijini Arusha.Amewaomba wananchi wa Arusha na wana-Kimadolu kujitokeza kupiga kura.Amesema sanduku la kura ndio sehemu sahihi ya kuimaliza CHADEMA na upinzani kwenye uchaguzi huu mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika kesho jumapili.Photo by Sanga Richard
Aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA na mtu wa karibu wa Mbunge wa Arusha Ndugu Niko,sasa ni mwanachama wa CCM amesema"Licha ya kuwepo dalili za kundi la Lema kuleta vurugu hapo kesho kwenye uchaguzi naomba wananchi mjitokeze mapema sana kupiga kura.Kwa wale wakristo tukitoka kanisani tukapige kura kwa mgombea wa CCM Bi.Edna Jonathan Saul.Photo by Sanga Richard
"Upinzani wamewafanyia nini?Huyo diwani wao anagombea ili aende Halmashauri akafanye nini?Sera na ilani inayotekelezwa niya CCM.Kumpeleka mpinzani halmashauri ni kutafuta kurudi tena kwenye hali ya maandamano na kelele ambazo hazileti maendeleo"Naibu katibu Mkuu CCM.Photo by Sanga Richard
Kazi na dawa.Pichani ni kijana aliyejitokeza kurudisha kadi ya CHADEMA Mbele ya Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara,Mh.mwigulu Nchemba.
Photo by Sanga Richard
Kijana akiwa amependeza kofia na kitambaa cha CCM,Huku Mh:Mwigulu Nchemba akionesha kadi ya CHADEMA kama ishara ya kupata mpiga kura mwingine kwenye uchaguzi wa kesho tar.16/06/2013 Photo by Sanga Richard
"Mmeionaaaaaaaa?Kijana amejitambua anarejea kwenye chama cha watu wenye nia na maendeleo,CCM chama cha kitaifa"Naibu Katibu Mkuu Mwigulu Nchemba Photo by Sanga Richard
Naibu katibu mkuu akisisitiza jambo."Naomba sana chukua muda wako kidogo tu nenda kapige kura ndipo uendelee na mambo mengine.Nendeni mkaipe ushindi CCM,Nendeni mkakaribishe maendeleo ndani ya kata ya kimadolu.Hao wapinzani wapo bize kupigania kuingia Halmashauri waende wakapambane na meya na sio kuwaletea maendeleo.Niambieni ni kitu gani hata kidogo tu walichowafanyia hao wapinzani hapa Arusha na kwenye kata yenu?"Mwigulu nchemba.Photo by Sanga Richard
Mamia ya Wanachi wakiwa na utilivu wa hali ya juu wakimsikiliza Naibu katibu mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba.Photo by Sanga Richard
Mh.Mwigulu nchemba akihitimisha mkutano wa hadhara kwa kumnadi mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM Bi.Edna saul.Nanukuu"Huyu ndiye diwani wenu mpya,kwa muda wa miaka miwili ijayo atawaletea maendeleo mliyoyakosa kwa miaka miwili iliyopita.Wakuamua kuwa yeye awe diwani hapo kesho ni nyie wanakimadolu kujitokeza kwa wingi kupiga kura".Photo by Sanga Richard
"Thamani ya kijana sio kiroba,kama kweli wanawathamini basi wasingekuwa wanazunguka na Helkopta angani zaidi ya Milioni 200 halafu wakishuka wanakuja kuomba miamia zenu.Huu ni upuuzi ambao manatakiwa kuukataa kwa kumchagua Bi.Edna Jonathan saul mgombea wa CCM."Photo by Sanga Richard
"Mamia ya Wananchi wakiwa na utulivu wa hali ya juu wakimsikiliza Naibu katibu mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba".Photo by Sanga Richard
"Tutawashindia hapa hapa.Wao wameshindwa kuwaheshimu wakamfukuza diwani.CCM itawapa diwani bora na kwamanufaa ya wanakimadolu na sio mtu binafsi".
Photo by Sanga Richard

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger