Mtoto Faith Warioba anayesoma katika shule ya awali ya Montessori jijini Dar es Salaam akimlaki kwa maua Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi nchini huku Rais Dkt.Jakaya Kikwete akishuhudia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi jana asubuhi Juni 27,2013 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa akisalimia na Msaidizi wa Rais Masuala ya Kidiplomasia,Balozi Liberata Mulamula wakati Rais Kikwete alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi na wasaidizi wake kwa mgeni wake muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi jana asubuhi Juni 27,2013 .
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa wakipokea heshima za urais muda mfupi baada ya mgeni huyo kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam jana asubuhi Juni 27,2013.
Rais wa Sri Lanka Me.Mahinda Rajapaksa akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana asubuhi Juni 27,2013 asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za utamaduni vilivyokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa shamrashamra za kumpokea mgeni huyo wakati alipowasili jana asubuhi Juni 27,2013 kwa ziara ya kikazi nchini.(picha na Freddy Maro + MICHUZI BLOG).
No comments:
Post a Comment