Thursday, June 27, 2013

MFALME MSWATI III WA SWAZILAND AWASILI DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mfalme Mswati III, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa ‘Smart Partnership’ unaotarajia kuanza Juni 28. Kushoto ni mke wa Mfalme Mswati.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkaribisha Mfalme Mswati wa (ii) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo.  Mfalme Mswati wa III ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa ‘Smart Partnership’ unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati ii, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Mfalme Mswati wa III, ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa ‘Smart Partnership’ unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.


Mfalme wa tatu wa Swatziland amewasili nchini jana na kupokelewa na mwenyeji wake makamu wa rais Dkt Ghalib Bilali aliyeambata na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe. Ujio huo wa Mfalme Muswati ni kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa ‘Smart Partnership’ unaotarajia kuanza Juni 28, 2013.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger