Sunday, June 23, 2013

PICHA:MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA KKKT


Picture
Picture
Picture





Picture
Picture

Washarika na watu mbalimbali wamejumuika leo katika maadhimisho ya miaka hamsini tangu kuunganika kwa makanisa saba ya Kilutheri nchini na kuunda Kanisa moja la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Kilele cha maadhimisho hayo yaloyoanza jana kinafanyika Jumapili ya leo, Juni 23, 2013 katika Dayosisi ya Kaskazini, usharika wa Chuo Kikuu cha Tumaini (TUMA - Tumaini University of Makumira), Makumira, Usa River, Arusha yakiongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Alex Gehaz Malasusa.

Watu wapatao 5,000 wanatarajiwa kujumuika katika maadhimisho hayo.

Wanahabari wa Redio Sauti ya Injili, Moshi Tanzania wakiripoti moja kwa moja kutoka katika viwanja hivyo, wanasema hali ya amani na utulivu vimetawala hadi sasa.

KKKT inatokana na makanisa yaliyoanza kutekeleza utume wa kueneza Injili zaidi ya miaka 100 iliyopita nchini Tanzania. Mnamo tarehe 19 Jini 1963, makanisa yaliamua kiweka nbali tofauti zao na kuunganika na kuunda Sinodi na baadaye Dayosisi. Hadi Mei 26, mwaka huu, KKKT imefanikiwa kuwa na Dayosisi 22 na Misioni 20 zinazotoa huduma mbalimbali za kiroho kwa washarika wake na huduma za kijamii kwa wote kama vile mashule, vyuo vya mafunzo ya ufundi, Vyuo vya Elimu ya Juu, mabenki, mahoteli, mahospitali n.k.

Viongozi wakuu walioiongoza KKKT hadi sasa ni:

  • Askofu Stefano Ruben Moshi (1963 - 1976)
  • Askofu Dk Sebastian Kolowa (1976 - 1992)
  • Askofu Samson Mushemba (1992 - 2007)
  • Askofu Dk Alex Gehaz Malasusa ( 2007 hadi sasa)
  • Maaskofu Moshi na Kolowa ni marehemu. 

  • Askofu Mushemba ni mstaafu.
Kwa hisani ya   HABARI MPASUKO

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger