Wednesday, July 24, 2013

ASKARI ALIYEUWAWA DARFUR AZIKWA SONGEA

SIMANZI ,Vilio,majonzi vilitawala katika mazishi ya askari wa Jeshi la Wananchi Rodney Ndunguru wa kikosi cha Makomando cha 92 KJ Ngerengere mkoani Morogoro - mazishi yaliyofanyika Mkoani Ruvuma.


Askari wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Rodney Ndunguru
habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com na MICHUZI

Aliye kaa katikati ni mama wa marehemu Rodney Ndunguru
habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com na MICHUZI

Picha ya marehemu Rodney Ndunguru wakati wakielekea katika makaburi ya Mjimwema
habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com na MICHUZI

Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Rodney Ndunguru wakati wakielekea katika makaburi ya Mjimwema
habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com na MICHUZI

Umati wa watu uliojitokeza katika mazishi ya Rodney Ndunguru katika makaburi ya Mjimwema .
habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com na MICHUZI

Umati wa watu uliojitokeza katika mazishi ya Rodney Ndunguru katika makaburi ya Mjimwema .
habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com na MICHUZI

Mwili wa Rodney Ndunguru ukiingizwa katika kaburi
habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com na MICHUZI

Mama wa marehemu Rodney Ndunguru akiweka taji katika kaburi la mwanaye
habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com na MICHUZI

SIMANZI ,Vilio,majonzi vimetawala wakati wa mazishi ya askari wa Jeshi la Wananchi Rodney Ndunguru wa kikosi cha makomando cha 92 KJ Ngerengere mkoani Morogoro ambapo mamia ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwemo askari wa Jeshi la wananchi ambao walihudhuria mazishi yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea.

Katika mazishi hayo ambayo yaliongozwa na Paroko wa kanisa katoriki jimbo kuu la Songea parokia ya Mjimwema padre Noel Duwe ambaye wakati akiendesha ibada ya mazishi aliwaonya Watanzania kutochezea amani na kwamba utulivu walionao watanzania unahitajika kulindwa kwa namna ya aina yeyote na si vinginevyo.

Padre Due alisema kuwa kwa wale wote wanaotaka kuchezea amani na utulivu tulionao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa kuwa watanzania hatujazoea vurugu wala umwagaji wa damu jambo ambalo lilionekana kuvuta hisia kwa watu waliofika kuomboleza msiba hu.

Aidha Padri Due alimfagilia waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano Mizengo Pinda kwa kauli yake aliyoitoa Bungeni kuwa kuwa jeshi la Polisi lihakikishe kuwa linawadhibiti watu wanaoleta fujo kwa kupiga na kwamba kauli yenye agizo hilo inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote badala ya kuibeza kwa kuwa hivi sasa watu wengi wamekuwa wakidharau vyombo vya Dola wakizani kuwa serikali haipo.

Kwa upande wake Kaimu wa Brigedi ya kanda ya kusini Kanari George Msongole alieleza kuwa taarifa ya kifo cha Rodney ilipokelewa muda mfupi baada ya kifo chake na kuwa Jeshi la wananachi linaungana na familia ya marehemu katika majonzi na msiba mzito.

Kwa upande wake msemaji wa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amesema kuwa familia imepata pengo kubwa kwa kuondokewa na kijana wao ,na ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuisaidia ili waweze kujengewa nyumba ambayo itwasaidia kwa kuishi mama yake mzazi na mjane.

Alisema kuwa Rodney Ndunguru amefariki akiwa na miaka takribani miaka saba kazini na akiwa na umri wa miaka 28 ambapo kimsingi kifo chake kimeacha pengo kubwa katika famila kwani katika uhai wake ilikuwa farja kwa ndugu na jamaa.

Rodney Ndungu amezikwa saa 10:45 jioni kwenye makaburi ya mjimwema ambako mamia ya wakazi ya mkoa wa Ruvuma walihudhulia akiwemo mwakilishi wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu ambaye ni katibu tawala ya wilaya ya songea Joseph Kapinga na kwamba mazishi yaliendeshwa kijeshi ambapo askari wote walikuwa wamevaa sare huku wakifunga vitambaa vyeusi kwenye mikono yao.
Na Cresensia Kapinga,Songea.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger