Thursday, July 11, 2013

Kenya yaongoza kwa ufisadi kati ya nchi 107

Kenya yaongoza kwa ufisadi

Yaongoza kwa ufisadi kati ya nchi 107 ambako utafiti huo ulifanyika,jambo ambalo limewasikitisha wakenya


Photo by Mwandishi wetu

1. Sierra Leone 84%

2. Liberia 75%

3. Yemen 74%

4. Kenya 70%

5. Uganda 61%

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Transparency International, Kenya imeshika nafasi ya nne kwa ufisadi ikiwa ni miongoni mwa nchi 107 ambako utafiti huo ulifanywa.

Ripoti hiyo ilibaini kwamba Wakenya saba kati ya 10 waliohojiwa walisema wamewahi kutoa hongo maishani mwao ili waweze kupata huduma moja hadi nane kati ya zilizochunguzwa.

Kulingana na utafiti huo, maofisa wa polisi ndio waliopatikana kuwa mafisadi zaidi nchini wakifuatiwa na wabunge, vyama vya kisiasa, mahakama na wafanyakazi wa Serikali.

Wakenya wengi walisema vyombo vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za kidini hazina ufisadi mwingi.

Nchi fisadi zaidi duniani ni Sierra Leone ambako asilimia 84 ya watu waliohojiwa walikubali kwamba wametoa hongo. Sierra Leone inafuatwa na Liberia (asilimia 75) na Yemen (asilimia 74).

Nchi ambazo zilipatikana kuwa na ufisadi finyu ni Finland, Japan, Australia, Denmark, Uhispania, Canada, Ureno, Uruguay, Norway, New Zealand, Korea Kusini na Malaysia ambako watu zaidi ya 95 kati ya 100 waliohojiwa walisema hawajaona ufisadi wowote nchini mwao.

Katika eneo la Afrika Mashariki, Kenya ndiyo nchi fisadi zaidi ikifuatwa na Uganda (asilimia 61) na Tanzania (asilimia 56).

Kulingana na utafiti huo ambao watu 114,000 walihojiwa, Rwanda ilipatikana kuwa na ufisadi mdogo zaidi katika eneo la Afrika Mashariki.

Raia 13 pekee kati ya 100 wa nchi hiyo walikubali mwamba wametoa hongo. Ufisadi ulipatikana kukithiri zaidi barani Afrika. Baadhi ya nchi fisadi zaidi Afrika ni Zimbabwe, Msumbiji, Libya na Cameroon (zote zikiwa na asilimia 62) na Nigeria (asilimia 44).

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger