Wednesday, July 24, 2013

MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA MAMA CHERRIE BLAIR

VIONGOZI NA WANAKIJIJI CHA HOYOYO WILAYA YA MKURANGA - MKOANI PWANI WAPATA FUTARI NA MAMA SALMA KIKWETE.


Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na mgeni wake Mama Cherrie Blair, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza walipokutana leo kwenye ofisi za WAMA tarehe 23.7.2013 Mama Blair yupo nchini akifuatana na mumewe Tonny Blair katika ziara ya kikazi.
Photo by Anna Nkinda - Maelezo na (Muhidin Michuzi)

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa nasaha zake baada kuwafuturisha viongozi wa serikali, madhehebu ya dini wa wilaya ya Mkuranga na wananchi wa kijiji cha Hoyoyo kilichoko karibu na Mkuranga katika Mkoa wa Pwani tarehe 23.7.2013.
Photo by Anna Nkinda - Maelezo na (Muhidin Michuzi)

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Cherrie Blair wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, mara baada ya kufanya mazungumzo yao.
Photo by Anna Nkinda - Maelezo na (Muhidin Michuzi)


Photo by Anna Nkinda - Maelezo na (Muhidin Michuzi)

Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuhubiri amani katika majukwaa yao ili jamii ielewe umuhimu wa kuwepo kwa amani na kuendelea kuishi kwa upendo na ushirikiano.



Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiwafuturisha wanakijiji cha Hoyoyo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Mama Kikwete alisema kuwa viongozi wa dini wanajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa waumini wao wanaelewa umuhimu wa amani katika nchi kwa kujenga mshikamano kama waasisi wa Tanzania walivyouanzisha .



“Katika shughuli yetu hii tumekusanyika watu wa dini mbalimbali wanaofunga mwezi huu na wengine mwezi mwingine lakini dua ni dua kupitia kwa mwanadamu yeyote Mwenyezi Mungu inamfikia, hivyo basi tuzidi kushikamana kwa kila jambo”.

Aliendelea kusema kuwa amani inatafutwa kwa miaka mingi, lakini inaweza kutoweka kwa muda mchache, hivyo basi kila mtu na hasa viongozi wa dini watumie muda wao kuhubiri umuhimu wa amani katika nchi na neno amani lisitoweke ndani ya vinywa vyao.

Kwa upande wake Sheikhe Athuman Kinyozi alimshukuru Mama Kikwete kwa futari aliyoiandaa kwa ajili yao na kusema kuwa mtu anayejitoa kwa ajili ya kufuturisha wengine anapata thawabu kwa Mwenyezi Mungu.

Sheikhe Kinyozi alisema kuwa kufanya kitendo cha kufuturisha si lazima uwe na uwezo mkubwa kifedha, bali unaweza ukanunua hata tende au maji na kuwapa watu waliofunga. Kile ulichowapa kikiwa ni kitu cha kwanza kutia midomoni mwao utalipwa thawabu za funga ya wale wote uliowapa kitu walichokula.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger