Miradi miwili ya maendeleo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma yote ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.6imezinduliwa
Waziri Mkuu Mizengo kayanza Pinda akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Hospital ya Wilaya ya Namtumbo
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa machinjio ya
kisasa katika mji mdogo wa Namtumbo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma
Baadhi ya Viongozi wakishangilia baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kukata utepe
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizundua mitambo ya kuzalisha umeme katika mji
mdogo wa Namtumbo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
WAZIRI Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda
ameweka jiwe la msingi na kuzindua miradi miwili ya maendeleo wilayani Namtumbo
mkoani Ruvuma yote ikiwa na thamani ya
zaidi ya shilingi bilioni 1.6.
Miradi hiyo iliyotembelewa
kuwekwa jiwe la msingi na kuzinduliwa
katika siku ya tatu ya ziara ya Waziri mkuu mkoani Ruvuma ni pamoja na hospitali ya wilaya
ya Namtumbo iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 600 kwa ujenzi uliofikiwa na itakapokamilika itagharimu
kiasi cha shilingi bilioni 4.4 huku akizindua mradi wa machinjio ya kisasa ya
mji wa Namtumbo ambayo yamegharimu kiasi cha shilingili milioni 148.
Katika hatua nyingine Waziri mkuu amewasha rasmi umeme wa
jenereta katika mji huo wa Namtumbo ambao ujenzi wake umegharimu kiasi cha
shilingi milioni 800 na kuwata wananchi
wilayani humo kuitumia miradi hiyo yote kujiletea maendeleo ambayo yanapaswa
kuibuliwa na wao wenyewe na serikali itatoa ushirikiano mkubwa katika kuifanya
wilaya ya Nmtumbo kuwa ya kisasa zaidi.
Amesema kuwa kuwepo kwa umeme,hospitali na huduma nyingine
za muhimu katika maendeleo kutawezekana kwa wananchi wenyewe kujituma katika
kufanya kazi zaidi na hsa katika kilimo cha mazao mbali mbali kwa sababu ardhi
ya wilaya ya Namtumbo inaruhusu kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
Amesema kuwa maendeleo
yoyote duniani huletwa na wananchi kwa kutumia ipasavyo fursa zilizopo
katika maeneo yanayowazunguka hivyo amewataka wananchi wilayani Namtumbo na
mkoani Ruvuma kwa ujumla kuzitumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo na
serikli itaunga mkono kwa dhati jitihada zozote za wananchi katika suala zima
la kujiletea maendeleo.
Aidha amesema kuwa dhamira ya maendeleo huanza kwa mwananchi
mmoja mmoja kwa kukubali kutumia fursa mbali mbali zilizopo katika eneo husika
na siyo kwa kukaa na kulalamikia serikali kwa kuitaka iwaletee maendeleo bila
wao kujishughulisha katika kuyatafuta maendeleo na amewataka wananchi kuitunza
miradi yote ya maendeleo iliyopo kwa ajili ya manufaa yao na kizazi kijacho.
Waziri mkuu amewataka kutambua kuwa miradi hiyo yote
imetumia gharama kubwa ambazozimetokana na kodi zao pamoja na wafadhili ambao nao wanatoa
kama msaada kutoka kwenye kodi za wananchi wao hivyo ni wajibu wa kila mmoja
kuithamini miradi hiyo kwa ajili ya maendeleo yao.
Picha na habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com
No comments:
Post a Comment