Friday, July 12, 2013

Mjadala mkali umeibuka katika bunge la Kenya

Mmea wa Miraa wazua mjadala bungeni Kenya

Biashara ya miraa imesheheni katika miji yote nchini Kenya image

Mjadala mkali umeibuka katika bunge la Kenya kuwa Mmea wa Miraa umesambaratisha maisha ya jamii, hivyo basi unapaswa kuorodheshwa kama Mihadarati mingine

Bunge la Kenya sasa limelazimika kuteua kamati ya wabunge 30 kuchunguza manufaa au madhara yanayotokana na utafunaji wa miraa, kufuatia madai kuwa imevunja ndoa nyingi.

Mamlaka inayohusika na mikakati ya kupambana na dawa za kulevya nchini Kenya -NACADA inaongoza kampeni ya kutaka Miraa (khat) ipigwe marufuku, wakisema ni mihadarati.

Jamii kutoka maeneo yanayopanda mmea huo kwa wingi, mfano jamii ya Meru katika mkoa wa Mashariki inasema kufanya hivyo ni kuwanyima kipato.

Wanalinganisha pato kutokana na Miraa na mapato ya jamii inayotegema mifugo kama ng'ombe, na sasa wabunge kutoka Meru wametetea zaidi kilimo cha Miraa.

Biashara ya miraa imesheheni katika miji yote nchini Kenya, na kuuzwa kwa wingi kwa watu wenye asili ya Kisomali Kaskazini Mashariki mwa Kenya na hata Somalia.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger