Sunday, July 21, 2013

ZIARA YA WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA SONGEA MJINI - Julai 20, 2013.

Katika ziara hiyo aidha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pia alikagua mabwawa ya kufugia samaki wakati alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya Ufugaji Samaki cha Ruhila kilichopo mjini Songea.

image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mabwawa ya kufugia samaki wakati alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya Ufugaji Samaki cha Ruhila kilichopo mjini Songea. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya uhamiaji wakati alipowasili kwenye jengo la Idara hiyo mjini Songea kuweka jiwe la msingi akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama chakula cha samaki wakati alipotembelea Kituo cha Maendeleo ya Ufugaji wa Samaki cha Ruhila kilichopo Songea Mjini akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013. Wapili kulia ni mkewe, Mama Tunu Pinda na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabit Mwambungu.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama moja ya magari ya mafunzo yanayotumika katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Tanzania (VETA) cha Songea wakati alipokizindua,Julai 20, 2013.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (wapili kuhoto) wakitazama vyakula na vifaa mbalimbali vya jikoni katika maonyesho ya kozi zinazofndishwa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Tanzania (VETA) cha Songea wakati alipokizindua Julai 2013.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Wairi Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakisalimiana na madiwani wa Manispaa ya Songea wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Songea akiwa kayia ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto kwake) wakitazama ngoma ya wanawake wa Songea kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea Julai 20, 2013.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanafnzi wa Shule ya Sekondari ya Songea Girls baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea Julai 20, 2013. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Baadhi ya Waislam walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye Ikulu ndogo ya Songea wakishiriki katika futari hiyo Julai 20, 2013.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya wanawake walioshiriki katika futari ambayo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwaandalia baadhi ya Waislam wa Songea Julai 20, 2013. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger