Mwenyekiti wa CCM ,Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula
(kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana wakiingia katika ukumbi
wa mikutano wa White House uliopo katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma
leo.Rais Kikwete amefungua na kuongoza semina kwaajili ya wajumbe wa
Halmashauri kuu ya CCM taifa ambayo pamoja na mambo mengine itachagua wajume wa
Kamati kuu.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete akielekeza jambo wakati wa ufunguzi wa Semina maalum kwaajili ya
wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa iliyofanyika mjini Dodoma katika ukumbi
wa White House makao makuu leo.Kushoto anayesikiliza kwa makini ni Makamu
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM bara Pius Msekwa.Wengine katika picha ni Rais Wa
Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed
Shein(Wapili kushoto),Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana(wanne
kushoto), na kulia ni Makamu Mwenyekiti CCm Bara Ndugu Philip Mangula
Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu
ya CCM taifa wakihudhuria semina maalum iliyofunguliwa na kuongozwa na
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa White
House,Makao makuu ya CCM mjini Dodoma.Picha na Freddy Maro.
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Wilson Mukama akisalimiana na
Katibu wa NEC, Oganaizesheni mstaafu Asha Abdallah Juma nje ya ukumbi kabla ya
kuanza semina. Mukama na Asha sasa ni Wajumbe wa NEC
Baadhi ya maofisa wa Chama wakiwa kwenye semina hiyo
No comments:
Post a Comment