Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela
akimenya muhogo ili kutafuna kidogo mara baada ya kununua kwa mmoja wa wakulima
Kijiji cha Nkungwe ndicho kinachoongoza kwa kilimo cha Muhogo mkoani Kigoma
Viongozi mbalimbali wakikagua kivuko cha Mto Ruchi katika
kijiji cha Nkungwe jana.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela
akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Kabanda katika kijiji cha
Chabwimba jana
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela
akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasili katika Kata ya Mabembe.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela
akivuka katika kivuko cha Mto Ruchi kwa kutumia Baiskeli huku akiwa ameonozana
na viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Kigoma Vijijini pamoja na watendajiwa
kijiji hicho jana inaelezwa kwamba watu wengi walipotea maisha kwa kuliwa na
Mamba kabla ya kujengwa kivuko hiki.
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kata ya
Mwanduga Kigoma vijijini jana
Mjumbe wa NEC CCM kupitia Wilaya ya Uvinza Asha Baraka akiwa
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mwanduga Kigoma jana kulia
ni Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Kigoma Vijijini na katikati ni Peter
Msanjila Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kigoma.
Martin Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akihutubia mkutano
wa hadhara uliofanyika jana kwenye kata ya Mwanduga Wilaya ya Kigoma vijijini
Huu ndiyo mto Ruchi unaotenganisha kijiji cha Nkungwe na
mashamba ya wanakijiji hao uliosababisha mauaji ya wananchi kadhaa kutoka na
kuliwa na Mamba kabla ya kujengwa kwa kivuko hicho.
Matin Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akipata maeleo
kutoka kwa Khamis Bitese Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati
alipotembelea na kukagua ujenzi wa madarasa
katika shule ya msingi ya Kabanda.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela
akikabidhiwa zawadi ya mihogo na Bi Asha Ibrahim mara baada ya kutembelea
shamba lake jana, .Kijiji hicho cha Nkungwe ndicho
kinachoongoza kwa kilimo cha muhogo bra katika mkoa wa Kigoma.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM, UVCCM Bw. Martin Shigela
akishiriki katika
kupalilia shamba la Karanga katika kijiji cha Nkungwe Tarafa
ya Mabembe Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembelea na kujionea shughuli
mbalimbali na kukagua
miradi inayotekelezwa na wananchi kwa pamoja na Serikali
jana.
Sekretarieti ya CCM ikiongozwa na katibu mkuu wa CCM Ndugu
Abdurahman Kinana iko mkoani Kigoma kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa Ilani
ya Chama cha Mapinduzi na sherehe za miaka 36 ya chama hicho zinazotarajiwa
kufanyika Februari 3 kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo, kulia ni Bi
Fatma mmiliki wa na kushoto ni Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigoma
Vijijini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela
akisalimiana na wananchi wa
kijiji cha Nkungwe wakati alipotembelea katika
kijiji hicho jana
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akimkabidhi zawadi ya shilingi elfu
10,000 mtoto Rehema huku mama yake akimsaidia wakati alipotembelea na kujionea
shughuli za kilimo katika kijiji cha Nkungwe jana
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela
akimsaidia Bi. Asha Ibrahim
kufukia mbegu ya Viazi, huku viongozi mbalimbali wa
CCM wilaya ya Kigoma Vijijini
wakishuhudia tukio hilo.
No comments:
Post a Comment