Saturday, January 26, 2013

MKUU WA MKOA WA DODOMA AONGOZA MAPOKEZI YA SEKRETARIETI LEO ASUBUHI

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akiongoza mapokezi ya ujumbe wa Sekretarieti ya CCM,unaoelekea mkoani Kigoma mapema asubuhi hii kwa usafiri wa treni,ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM yatakayo adhmishwa mkoani humo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na Wanachama wa CCM mkoani Dodoma waliokuwa wamefika Stesheni ya Dodoma asubuhi hii kuwalaki Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka jana jijini Dar kwenda Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.Kushoto kwake ni Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na kulia kwake ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya WanaCCM wa Mkoani Dodoma waliofika kuwalaki na kuwatakia safari njema Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka jana jijini Dar kwenda Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.
 Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi CCM Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika stesheni ya treni Mkoani Dodoma leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger