Saturday, January 26, 2013

MSAFARA WA KINANA UNAOSAFIRI KWA TRENI DAR-KIGOMA WAFIKA TABORA JIONI YA JUMAMOSI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinunua mishikaki kwa mmoja wa wauzaji wa vyakula mbalimbali husuasan nyama, baada ya kuwasili na msafara wake stesheni ya Saranda, mkoani Singida, leo mchana. Kinana na msafara wake wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, wanasafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam, kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. (Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai. (Picha na Bashir Nkoromo)

 Makatibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia) na wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kulia) wakinunua chakula kwa mamalishe, kwenye stendi ya Saranda mkoani Singida, daaba ya kuwasili kwenye stesheni hiyo, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM.(Picha na Bashir Nkoromo)

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mstaafu John Chiligati wakishiriki kucheza ngoma ya wakazi wa mkoa wa Singida, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Martine Shigela.(Picha na Bashir Nkoromo).
Katibu Mkuu wa CCM, akisalimiana na wananchi wa Itigi.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipuliza filimbi kuchangamsha ngoma aliyokuwa akishiriki kucheza na wananchi wa mkoa wa Singida, katika burudani ya ngoma iliyotolewa, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM.(Picha na Bashir Nkoromo)
Ujumbe wa Sekretarieti ukisalimiana na Uongozi wa Tabora mara baada ya kuwasili hapo wakiwa njiani kuelekea Kigoma kwa kutumia usafiri wa Treni ya Reli ya kati.
Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wananchi wa  Saranda, tarafa ya Kilimatinde, Wananchi wamefurahi kuona viongozi wao wakiwa nao pamoja na kusafiri nao pamoja.
Shughuli za kila siku eneo la Stesheni ya  Saranda.
 
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahaman  Kinana, na  Mbunge wa Manyoni Mashariki, Kepteni Mstaafu John Chiligati wakila mishikaki  baada ya kuwasalimu wana CCM  katika stesheni ya Saranda.

Wadau  wa Habari wakiwa kazini ndani ya behewa kuelekea Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM
Treni ya iliyobeba wajumbe wa Sekretarieti na wananchi wengine ikielekea Kigoma.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger