Sunday, January 27, 2013

MSAFARA WA KATIBU MKUU WA CCM WAKUTANA NA WANACHAMA WA CCM MANYONI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahmani Kinana akizungumza na Wana CCM wa Manyoni leo.

Vijana wa Chipukizi Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida wakimvisha skafu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Abdulrahmani Kinana alipofika kwenye kituo cha treni cha Saranda mkni humo na kuzungumza na wanaCCM wa Manyoni. Ndg.kinana na ujumbe wa Sekretarieti ya CCM wako safariniu kuelekea Mkoani kaaadhimisho ya Miaka 36 ya CCM.
Katibu wa NEC , Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na wanaCCM wa Manyoni leo.


Katibu wa NEC , Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dkt. Asha Rose Migiro akiwasalimia wanaCCM wa Manyoni.
Mbunge wa Jimbo la Manyoni, Ndg. John Chiligati akizungumza.
Katibu wa NEC , Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, dt. Asha Rose Migiro akiwasalimia wanaCCM wa Manyoni, Mkoani Singida, waliposimama katika kituo cha Saranda.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahmani Kinana (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Tabora waliofika kwenye stesheni ya treni ya Mkoa huo kuupokea ujumbe wa Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, unaoelekea Mikoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha mapinduzi (CCM)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahmani Kinana sambamba na Katibu wa NEC,Itikadi na uenezi CCM, Nape Nnauye wakiwaaga Wanachama wa CCM maeneo ya stesheni ya Saranda, Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida,wakiwa na wajumbe wa Sekretarieti  ya CCM unaoelekea Mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Bai bai......  !!! hivi ndivyo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Ndg Abdulrahmani Kinana sambamba na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM , Nape Nnauye walivyokuwa wakiwaaga wana CCM wa Mji wa Saranda, Wilayani Manyoni.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger