Wananchi wa Rungwe Juu na
Asante Nyerere wakishiriki kwa
wingi kwenye mapokezi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Ndugu Nape Nnauye
alipowasili Rungwe Kata ya Asante Nyerere.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipokewa kwa
mapokezi makubwa ,kulia kwake ni Mjumbe wa NEC wilaya ya Kasulu,Ndugu Daniel
Nswanzigwanko
Vijana wa Kata ya Asante Nyerere nao hawakuwa nyuma katika
mapokezi ya kiongozi wao wa Kitaifa.Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Nape Moses
Nnauye.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiweka jiwe la msingi la ujenzi
wa Ofisi za Chama Kata ya Asante Nyerere wilaya ya Rungwe.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi kata ya Asante Nyerere
,Ndugu Yohana ,akiwahutubia wananchi wa kata hiyo kwamba amerudi rasmi
nyumbani,pamoja na yeye wapo wengine wengi wamerudisha kadi zao akiwemo Katibu
wake Ndugu Frank Ignas Mudala,kadi zao zilirudishwa kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya Asante Nyerere ambapo Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi alihutubia.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia
wananchi wa wilaya ya Rungwe ,kata ya Asante Nyerere na kuwaambia wasifanye
makosa katika kuchagua viongozi, wachague viongozi wenye sifa,wapenda maendeleo
na wanaojali wananchi na kuelewa thamani ya amani ya nchi yetu.
No comments:
Post a Comment