Wananchi wa rika zote wa Kijiji cha Rumashi, Kata ya Nyabibuye, wilayani Kakonko, Kigoma wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahma Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika , Januari 30, 2013,katika kijiji hicho, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua soko la Kata ya Nyabibuye, Kakonko Januari 30, 2013, ikiwa ni ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma. Kushoto ni diwani wa kata hiyo Steven Mnigakiko na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kakonko Peter Toima.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa daraja la Umoja linalounganisha Kata ya Nyabibuye, Kakonko na vijiji jirani vya Burundi. alipokuwa katika ziara wilayani Kakonko Mkoani Kigoma, Januari 30, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu inayoambana na maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 3, mwaka huu mjini Kigoma.
Kinana na ujumbe wake wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa daraja hilo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo, alipofika kwa ajili ya kushiriki ujenzi wa nyumba ya walimu. Pia Kinana ameahidi kuipa shule, Mashine mbili za umeme wa Solar na kompyuta.
Kinana akipanda mti kwenye shule ya sekondari ya Nyamtukuza, katika Kata ya Nyabibuye wilayani Kakonko mkoani Kigoma. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Amani Ntibakiza
Wanafunzi wa shule hiyo wakisomba mawe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu
Kinana akishiriki kusomba mawe kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu katika shule hiyo
No comments:
Post a Comment