Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa |
Lowassa achangia Machinga Mwanza Sh20 milioni
Akizungumza na Wamachinga hao, Lowassa alisema jukumu la kuwasaidia Machinga linapaswa kuwa la wafanyabiashara wote na kwamba, iwapo hawatasaidiwa hawatakuwa salama.Mwanza. Waziri Mkuu aliyejiuzuru, Edward Lowassa, ametoa Sh20 milioni kusaidia wafanyabiashara ndogondogo maarufu Machinga wa Mtaa wa Makoroboi, ili kuwajengea uwezo wa kukuza mitaji ya biashara zao.
Akizungumza na Wamachinga hao, Lowassa alisema jukumu la kuwasaidia Machinga linapaswa kuwa la wafanyabiashara wote na kwamba, iwapo hawatasaidiwa hawatakuwa salama.
“Hamuwezi kuwa mnakimbizana nao Machinga kila uchao hawa, wawekeeni mazingira safi, wafanyabiashara mnayo sababu za kuwachangia, msipowachangia mjue watakula sahani moja nao,” alisema Lowassa.
Alisema Machinga lazima wachangiwe ili nao wafaidi matunda ya nchi na kwamba. jukumu la kuwachangia linapaswa kufanywa na wafanyabiashara wakubwa wa Mwanza.
“Wasaidie nao wale…tupishane kula wengine tutakula mkate na wao mhogo, lakini lazima wote wale,” alisema Lowassa.
Alisema kiwango alichochangia ni kama cha kusaidia Machinga wa Makoroboi, aliomba kuandaliwa kwa hafla kubwa kwa ajili ya kuchangia Sh1 bilioni kwa ajili ya Machinga wote Mwanza.
Lowassa alisema jukumu la kuandaa hafla nyingine kupata Sh1 bilioni amelikabidhi kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM, Dk Raphael Chegeni, Mbunge wa Kwimba, Shanif Mansoor, Mkurugenzi wa Nyanza Bottling Co. Ltd, Chrstopher Gachuma Artaf Mansoor ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya Moil.
“RPC ukitaka kukomesha wezi mjini kaa na machinga kuwasaidia, wanawajua wenzi hawa... wasaidieni maana mkiwasaidia mnatekeleza ilani ya CCM,” alisema.
Na Frederick Katulanda
UMEFIKA WAKATI SASA WA KUJENGA TAIFA LENYE NIDHAMU, NA BIDII KATKA KUYAFIKIA MALENGO YA MILENEA,KUTEKELEZA MALENGO YALIYO KATIKA DIRA YA TAIFA BILA UBABAISHAJI,KUONDOKANA NA BAJETI TEGEMEZI KWA MAENDELEO YAETU,NIDHAMU KATIKA MATUMIZI SAHIHI YA RASILIMALI ZA TAIFA HILI,NA KUONDOA MITIZAMO DUNI NA FIKRA POTOFU KATIKA SIASA ZA UDINI,UKABILA NA MAKUNDI YA KILA AINA.TUMCHAGUE KIONGOZI AMBAYE ANAWEZA KUSIMAMIA HAYA KWA UKAMILIFU NA UTHABITI.HUYU NI KIONGOZI YEYOTE MWENYE TABIA KAMA YA WAZRI MKUU MSTAAFU Mh" EDWARD LOWASA "
ReplyDelete