Thursday, January 24, 2013

TANZANIA YAPONGEZWA KWA KUTATUA MIGOGORO AFRIKA

Jukwaa la Mabunge ya kimataifa ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu  (FP-IOGLR) limeitaja Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kwa juhudi inazozifanya kuleta amani barani Afrika.

Pongezi hizi zimetolewa leo na jumla ya nchi kumi na mbili zinazounda Jukwaa hilo kwenye Mkutano wa tatu unaoendelea kwenye Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimewataja Rais Mstaafu Benjamin mkapa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Watanzania kama wapenda amani barani Afrika.

Hii ni kutokana na viongozi hao kujitolea kusuluhisha migogoro ya DRC / Rwanda na kundi la M23, migogoro ya Afriuka ya Kati, mgogoro wa Sudani Kusini, mgogoro wa Kenya baada ya uchaguzi mkuu na mingine mingi. Pamoja na tanzania frika Kusini na imepongezwa.

Bunge la Tanzania limewakilishwa na Spika wa Bunge ambaye ameongoza ujumbe wa wabunge watano ambao ni Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Pauline Gekul na Mhe. Sadifa Juma. Wengine ni Mhe. Mohamed Mbarouk na Mhe. Prudenciana Kikwembe.
 
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kupokelewa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo Bwana Hemed Mgaza (katikati) Kushoto ni Mwenyekiti wa Bunge na Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (Mb), kulia ni Mhe. Sadifa Juma Khamis, (Mb). Mhe. Spika ameongoza ujumbe wa Wabunge watano kuhudhuria mkutano  wa tatu wa Kimataifa  wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
 Spika wa Tanzania  Mhe. Anne Makinda na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende (kulia) wakiingia kwenye mkutano huo.

Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa PF-ICGLR (Forum of Parliaments of International Conference on Great Lakes Region FP/ICGLR) Mjini Kinshasa.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger