Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi [CCM] katika Manispaa ya Moshi (UVCCM) umeiomba serikali mkoani Kilimanjaro kuwachukulie hatua za kisheria baadhi ya viongozi wa Chadema wanaotumia lugha za matusi na kashfa dhidi ya viongozi wa serikali mkoani hapa.
Ombi hilo limo katika moja maazimio yaliyotolewa na baraza kuu la umoja huo katika manispaa hiyo kufuatia matusi na kashfa hizo zilizotolewa na viongozi wa chadema katika mkutano wao uliyofanyika hivi karibuni mjini moshi.
Katibu wa UVCCM Manispaa ya Moshi Joel Makwaiya amesoma maazimio ya kikao hicho mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama na kueleza kuwa viongozi hao katika mkutano huo wamewahamasisha wanachama wao wawapige makofi viongozi hao.
Makwaiya amewataja viongozi wanaokashfiwa na kutakiwa kupigwa makofi kuwa ni pamoja na Mkuu wa Mkoa Gama, mkuu wa Wilaya ya Moshi Dr Ibrahimu Msengi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Bi Benardeta Kinabo.
Hata hivyo Gama amewataka vijana hao kuwa wavumilivu na wasijiingize katika dimbwi la umwagaji damu kwa kuwa viongozi hao wa Chadema ndio upeo wao wa kisiasa na wananchi wanatakiwa wawaelewe hivyo na ndio wanaokimbilia madaraka ya nchi.
No comments:
Post a Comment