Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa mkoa wa
Lindi waliohudhuria sharehe za kutimiza miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi
zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo kata ya Chiponda mkoani Lindi
tarehe 5.2.2013.
Mjumbe wa NEC na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe
akimvisha skafu Bwana Omary Issa kutoka Chama cha Wananchi, CUF, akiwa ni miongoni mwa wanachama wapya waliojiunga na CCM kutoka
vyama vingine vya siasa wakati wa kilele cha sherehe za
kutimiza miaka 36 ya
kuzaliwa chama hicho.
Viongozi wa CCM Wakiongozwa na Mama Salma Kikwete wakikata keki kuashiria
kuzaliwa kwa chama hicho
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akifungua
rasmi jengo la CCM Tawi la Rondo kata ya Chiponda huko Lindi
Vijijini wakati wa kilele cha sherehe ya kutimiza miaka 36 ya CCM
zilizofanyika kimkoa kijijii hapo tarehe
5.2.2013. Kulia kwa Mama Salma ni Mjumbe wa NEC Taifa, Mbunge wa Mtama na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe.
Mama Salma Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe za
kutimiza miaka 36 ya CCM Mkoani Lindi akijumuika na wacheza ngoma ya Linyamwa
kucheza ngoma hiyo. Sherehe hizo zilifanyika katika
kijiji cha Rondo huko Lindi
vijijini
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba kutoka
kwa mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa kilele cha kutimiza miaka 36 ya
ChamaCha Mapinduzi. Sherehe
zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo Kata ya Chiponda huko Lindi vijijini.
Wanachama wa ccm wakisikiliza hotuba ya Mjumbe wa Nec,Mama Salma Kikwete
Mjumbe wa NEC Taifa kutoka wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma
Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM mwanachama mpya ambaye jina lake halikuweza
kufahamika mara moja wakati wa sherehe za kutimiza miaka 36 ya chama hicho.
Mjumbe wa Nec,Mama Salma Kikwete akifurahia burdan iliyokuwa inatolewa
na Wasanii katika sherehe za CCM.
Ngoma ya Linyamwa ya kabila la Wamwera ikichezwa na
wananchi wa kijiji cha Mpenda kutoka
wilaya ya Lindi vijijini wakati wa kilele cha sherehe ya kutimiza miaka
36 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi.
|
No comments:
Post a Comment