Azoa vigogo kibao wa Chadema.
Awafananisha na nguruwe anayekula watoto wake mwenyewe.
Awakumbusha upinzani si kupinga kila kitu.
Asema wananchi
wanakerwa na fujo zao bungeni.
Adai zitapunguza
idadi ya wabunge wao bungeni.
Zitashusha hadhi yao
kwa umma.
Asema walitumwa kutetea wananchi, si kufanya fujo.
Awaambia kazi ndo kwanza imeanza.
Adai miaka 20 inatosha kuwakomaza.
Juliana Shonza akihutubia wakazi wa Temeke juu ya maamuzi
yake thabiti ya kujiunga na CCM
Mtela Mwampamba akiwaeleza wananchi wa Temeke mapungufu
makubwa ya kidemokrasia yaliyopo kwenye vyama vya upinzani na hivyo kumfanya
yeye binafsi kuchukua uamuzi wa kujiunga na CCM.
Saumu Kisena akionyesha kitambulisho chake , Saumu amejiunga
rasmi CCM baada ya kugundua chama alichokuwepo kinahubiri haki nje wakati ndani
hamna haki kabisa.
Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi, akihutubia wananchi wa
Wilaya ya Temeke na kuwahakikishia kuwa CCM itaisimamia serikali itekeleze
ilani yake ya Uchaguzi kwa asilimia 100.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke ,Ndugu Sophia Mjema akiwapungia
wananchi wa Temeke wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
Pile ,Temeke ,Mwisho.
Wananchi na Wapenzi wa CCM kutoka kata ya Kilakala,Yombo
kama walivyojitambulisha ,walisema Nape ameongea mambo mengi ya msingi na
kumtakia heri aendelee kufanya kazi nzuri.
Wasanii wa kikundi cha TMK wakitoa burudani kwenye uwanja wa
nyumbani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile,
Temeke,tarehe 16/2/2013.
Baadhi ya wananchi wakionekana kuelewa vizuri maneno ya
viongozi wao.
Kikundi cha Hamasa cha CCM,Temeke kikihamasisha kwa aina
yake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pile,Temeke.
Ndg. Nape ameyasema hayo jana kwenye mkutano mkubwa wa
hadhara kwenye viwanja vya mwembe yanga Temeke wakati akihutubia maelfu ya
wanachi na mashabiki wa chama hicho kwenye mkutano huo.
Mkutano huo umeandaliwa na CCM mkoa wa Dar es salaam kwa lengo la kujibu mapigo ya
Chadema waliofanya mkutano wao siku ya jumapili.
Nape alisema, " watani zangu acheni kujiliza kila siku,
mnaishia kulialia tu. Mmekuja mwembe
yanga nikadhani mna jambo la maana,kumbe kulialia tu! Yaani miaka ishirini ya
vyama vingi bado mnajiliza tu? Mtakua lini?"
Nape akawndelea kusema kuwa uteuzi wa kamati kuu ya CCM ni
ishara kuwa kazi imeanza,hivyo kujiliza kwao hakuta irudisha nyuma CCM.
" Tumekamilisha uchaguzi na upangaji wa safu ndani ya
chama. Safu hii ina kazi kubwa mbili, kwanza kusukuma utekelezaji wa Ilani ya
uchaguzi ili kuboresha maisha ya watanzania na kazi ya pili ni kuhakikisha CCM
inashinda kwa kishindo 2014 na 2015"! Alisisitiza Nape
Akasema Chadema wameshindwa kukomaa mpaka sasa hata baada ya
miaka 20 ya mfumo wa vyama vingi kwasababu wana tabia ya nguruwe ya kula watoto
wake yenyewe.
" hawa watani kinachowamaliza ni kuwa na tabia ya
nguruwe, nguruwe akishazaa watoto, akishikwa njaa hula watoto wake mwenyewe,
sasa wao kila kukicha wanakula watoto wao wenyewe watakomaa lini?"alihoji
Nape.
Nape anasema kwasababu ya kutokomaa kwa upinzani nchini ndo
maana wamejenga tabia ya kupinga kila kitu hata yale yenye manufaa kwa
wananchi.
"Mtashangaa kuwa wenzetu hupinga kila kitu cha serikali
mpaka bajeti ambazo pesa zikipitishwa ndio zinajenga miundo mbinu kama
barabara, zinaleta madawa, zinaajiri waalimu, zinalipa mishahara na hata posho
wanazolipwa zinatokana na bajeti ya serikali, kwasababu ya tabia ya nguruwe kula
hata watoto wake ilimradi ana njaa, basi wao hupinga kila kitu" alisema
Nape.
"Angalieni bunge la bajeti mwezi wa nne mpaka wa saba,
mtagundua hakuna mpinzani atakubali bajeti ya serikali, ambayo pesa ikipitishwa
inakwenda kwenye majimbo yao pia. Bajeti iliyopita ni mpinzani mmoja tu nadhani
alikubali bajeti ipite." Alieleza Nape.
Aidha Nape alisema kwenye kikao cha NEC kilichomalizika
mjini Dodoma hivi karibuni pamoja na mambo
mengine walijadili changamoto kubwa ya ajira nchini hasa kwa vijana na kuahidi
kuwa swala hilo
atalizungumzia kwa kina kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika Goba leo jioni.
No comments:
Post a Comment