Katibu wa NEC
,Itikadi na Uenezi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari
Dodoma na kuwajuza mambo mbali mbali
yanayotarajiwa kufanyika kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu wa CCM.
Katibu wa NEC Itikadi
na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo,tarehe 9/2/2013 Dodoma.
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
Chama Cha Mapinduzi itafanya Mkutano wake wa kawaida kuanzia tarehe 10 -11
/02/2013. Kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dr. Jakaya
Mrisho Kikwete.
Wajumbe wa NEC wanatarajiwa
kufika Mjini Dodoma
leo tarehe 9/02/2013,kwa ajili ya kikao hicho.
Pamoja na mambo mengine kikao
hichi kitatanguliwa na Semina ya siku mbili kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa.
Lengo la Semina hii ni
kuwaongezea Wajumbe uelewa kuhusu masuala ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali
yake hasa ikizingatiwa kwamba wengi wa Wajumbe ni wapya kufuatia Uchaguzi Mkuu
wa CCM wa mwaka 2012.
Mada zitakazowasilishwa kwenye
Semina ni pamoja na;
1. Nafasi na Wajibu wa Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa
2. Umuhimu wa Maadili kwa
Viongozi na Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi.
3. Mikakati ya kutekeleza
maazimio ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa nane wa CCM.
4. Mkakati wa kukuza ajira
nchini.
Semina hii itafuatiwa na Mkutano
rasmi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambao pamoja na mambo mengine utafanya
Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi.
Imetolewa:
Nape Moses Nnauye
KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI
No comments:
Post a Comment