Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa
kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa
hadhara katika kijiji hicho leo, Feb 16, 2013.
Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimiana na watoto wa
kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa
hadhara katika kijiji hicho leo, Feb 16, 2013.
Mkazi wa Kijiji cha
Ng'apa wilaya ya Lindi mjini, akionyesha kadi yake ya matibabu ya Huduma ya
Kadi ulkiopo chini ya Bima ya Afya, wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa
na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
katika kijiji hicho, leo Feb 16, 2013. Mama Salma Kikwete alimpatia fursa ya
kuzungumza wakati akihimiza umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo wa
matibabu.
Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amegoma kushuka
katika gari lake, kukataa kwenda kwenye mkutano wa ndani wa Chama Kata ya
Tandangongoro, uliokuwa umepangwa na viongozi wa kata hiyo kufanyika katika
chumba cha darasa la shule ya msingi ya kijiji cha Ng'apa, mkoani Lindi, leo
Februari 16, 2013. Hatua hiyo iliwalazimu viongozi kutafuta ukumbi mwingine wa
dharura. Mama Salma alisema si sahihi mkutano wa ndani wa Chama cha siasa
kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya serikali
Umati wa wananchi wa Kijiji cha Ng'apa wakimsiliza Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akilipowahutubia mkutano wa hadhara leo, Feb 16, 2013. PICHA ZOTE NA BASHIR
NKOROMO).
No comments:
Post a Comment