Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg Mary Chatanda akipandisha bendera ya Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kuzindua Shina la wakereketwa wa CCM mtaa wa Olepolos, Tawi la Engira Kata ya Lemara leo 01/03/2013. Kushoto kwake ni Katibu wa Chadema wa Tawi Ndg Peter Sarangei (mwenye miwani) aliyerudisha kadi yake na kuamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg Mary Chatanda akiendelea kupandisha bendera ya Chama Cha Mapinduzi akishuhudiwa na umati mkubwa wa Wanachama wa Chadema na Mwenyekiti wa Chadema Ndg Tom (aliyeshika kipaza sauti) wa Tawi la Engira mara baada ya kupokea kadi za CCM leo 01/03/2013
Aliyekuwa Katibu wa Chadema wa Tawi la Engira,Ndg Peter Sarangei mara baada ya kurudisha kadi yake kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg mary Chatanda akipewa mkono wa pongezi na Viongozi wa CCM walioambatana na Katibu huyo.Kushoto kwa Katibu wa Mkoa ni katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg.fredrick Sabuni wakishangilia.
Hivi ndivyo Shina la Wakereketwa la Mtaa wa Olepolos lionekanavyo mara baada ya uzinduzi.
Wakazi na Wanachama waliokusanyika leo kumsikiliza na kushuhudia baadhi ya Wanachama wa Chadema wakirudisha kadi na kuamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Pichani (kuanzia kushoto) ni aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum kupitia Chadema Ndg. Rehema aliyejiunga na CCM,Katibu wa CCM Kata ya Lemara Ndg Happy Marandu akifuatiwa na Diwani wa Kata ya Lemara (CCM) Ndg Karimu Mushi mbele yake mwenye skafu shingoni ni Mwenyekiti wa UVCCM (CCM) Wilaya ya Arusha Ndg Martin Munisi (kushoto kwake ) ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa Ndg loth Oelevo na kulia kwake ni Katibu wa WAZAZI - CCM Wilaya ya Arusha Ndg Mdoe wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
Chama Cha Mapinduzi jijini Arusha kimeisambaratisha ngome ya Chadema katika Kata ya Lemara baada ya kuwachukua wanachama 85 wa Tawi la Olepolosi na kusababisha Tawi hilo kufungwa.
Miongoni mwa wanachama Chadema waliokihama na kukabidhiwa kadi za CCM na JEMBE Mary Chatanda leo ni Mwenyekiti wa Tawi hilo Heri Tom na Katibu wake Peter Sarangei.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi zao, Tom na Sarangei walisema kuwa, wamechukua uamuzi huo kutokana na Chadema na Mbunge wa arusha , kukosa mwelekeo na kubaki na maandamano na kuchochea vurugu kila kukicha.
Nae Chatanda aliwataka vijana hao kusahau vurugu za Chadema na kufuta sera nzuri za CCM na kujiunga na vikundi ili kuwarahisishia kupata mitaji ya kuendeshea shughuli zao za kibiashara. Pia Jembe Chatanda na Diwani wa Kata Lemara Ndg Karim Mushi walitoa pikipiki moja na pesa taslimu shilingi laki 3 kwa Shina hilo jipya, lilozinduliwa leo.
No comments:
Post a Comment