Ijumaa, March 15, 2013
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na
ujumbe wake, wakionyweshwa maumbo ya namna kiwanda cha viatu cha Huajian mjini
Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika
ziara ya mafunzo, nchini China. (Picha na Bashir Nkoromo).
Wafanyakazi wa Kiwanda cha viatu cha Huanjian, Dongguan, wakiwa kazini. |
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake,
wakipata maelezo kwa video, kuhusu kiwanda cha viatu cha Huajian mjini
Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika
ziara ya mafunzo, nchini China. (Picha na Bashir Nkoromo).
Alhamis, March 14, 2013
Alhamis, March 14, 2013
KITUO CHA WAJARIAMALI WASOMI CHA CHENGDU CHAMKUNA KINANA
NA BASHIR NKOROMO, CHENGDU, CHINA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema, Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kitaihimiza serikali yake, kuiga mbinu zinazotumiwa na Chama
Cha Kikomunisti cha China (CPC) ya kuweka vituo vya vijana wajasiriamali
wasomi, kuwezesha wanaomaliza elimu ya juu waweze kutumia vipaji vyao kujiajiri
badala ya kusubiri kuajiriwa.
Tanzania ikifanikiwa kufanya hivyo, itajikomboa kwa
kuwasaidia vijana wengi ambao baada ya kumaliza masomo huhangaika kutafuta kazi
za kuajiriwa badala ya kijiajiri wenyewe kutokana na elimu, ujunzi na ubunifu
walio nao.
Kinana alisema, hayo leo Machi 14, 2013 baada yeye na ujumbe
wake wa watu 14, waliopo katika ziara ya siku kumi ya mafunzo nchini China,
kutembelea Kituo cha vijana wajasiriamali cha Chengdu, jimbo la Sichuan na
kushuhudia jinsi vijana wasomi walivyoweza kutumia vipaji vyao kujiajiri baada
ya kukusanywa kwenye kituo hicho kinachoitwa, Chengdu Hich Tech Postgraduetes
Enterpreneurial Park.
"Kwa kweli vijana hawa wanaonyesha umahiri mkubwa wa
kutumia vipaji vyao, ni muhimu nasi tukaiga namna hii bora ya kuwaweka vijana
pamoja, kwa sababu inasaidia kupunguza tatizo la ajira na pia kuleta faida kwa
taifa", alisema Kinana.
Kinana alimwagiza Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM
(UVCCM) Martine Shigela aliyeko kwenye msafara wake, kuwasiliana na uongozi wa
kituo hicho ili kuona namna mbinu zinazotumika kuwakusanya vijana kwenye kituo
hicho zitakavyoweza kufanyika Tanzania.
Katika ziara hiyo, Kinana na msafara wake, walivutiwa baada
ya kushuhudia vijana wanavyobuni na kutengeneza vifaa vya kielekroniki kama vya simu, redio,
televisheni, na wengine kubuni katuni, michezo na manjonjo mbalimbali ambayo
huwekwa katika kompyuta na simu za mkononi kwa ajili ya wenye vifaa hivyo
kujiliwaza.
"Kwa hiyo zile 'game' ambazo huwa tunacheza kwenye simu
zetu au kompyuta ndiyo hutengezwa hapa?," aliuliza Katibu Mkuu wa Umoja wa
Vijana wa CCM, Shigela.
Akizungumza wakati akitoa maelezo kuhusiana na kituo hicho,
Mkuu wa Kituo hicho, Zheng Xiola alisema, vijana zaidi ya 100 wameweza
kukusanywa kwenye kituo hicho kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali za ubunifu
katika mambo ya teknolojia hasa kuhusu elekroniki.
Alisema, wakati wapo wanaobuni na kutengeza vifaa vya
kielekroniki kama vya simu, redio, televisheni na vifaa vingine vinavyotumia
umeme, wengine ni wabunifu na watengezaji wa vikatuni, michezo, na mamnjonjo mbalimbali
kwa ajili ya kompyuta au simu.
Xiola alisema, kazi hizo zimewafanya vijana wengi
wanaomaliza masomo ya elimu ya juu, kujiari kwa njia hiyo kwakuwa kazi zao
huuzwa ambapo kwa wale wanaotengeneza katuni, michezo na manjonjo ya kwenye
simu au kompyuta huweza kuuza kwa kampuni zinazoteneza vifaa hivyo na
wanaotengeneza vifaa vya kielekroniki huweza kuuzia kampuni au watu binafsi.
Alisema, mpango huo umetengezwa na serikali ya Chama Cha
Kimomunisti cha China, kwa kutengea fedha ambazo hukopeshwa wajasiriamali
wanaotaka kujiunga.
Pamoja na kituo hicho, leo Machi 14, 2013, Kinana na ujumbe
wake walitembelea pia maeneo mbalimbali katika mji wa Chengdu kwa lengo la
kuona na kujifunza fursa zipi CCM inaweza kuielekeza serikali yake, kuzifanya
kwa ajili ya kuwezesha Tanzania kuinuka kiuchumi kama nchi na pia wananchi wake
kwa jumla.
Baada ya kituo hicho, walitembelea eneo la kumbukumbu la
Kihistoria la Jin Sha kuona namna ambavyo kumbukumbu zinatunzwa kwa njia bora
zaidi ili kuwa na manufaa kwa taifa na dunia kwa jumla, pia walitembelea eneo
la kiutalii la kihistoria ya zaidi ya miaka 100 iliyopita la Kuan and Zai Culture alley ambako kuna
majengo na mandhari ya amiaka mingi ambayo huvuta walii.
Baadaye Kinana alikutana na Naibu Katibu Mkuu wa CPC jimbo la
Sichuani Zang Ning, na kuwa na mazungumzo naye kabla ya chakula cha jioni
katika hoteli ya Jinjiang mjini Chengdu.
No comments:
Post a Comment