Kituo cha kimataifa cha mikutano AICC kilichopo jijini Arusha |
Na Fidelis Butahe, Mwananchi
KWA UFUPI
Wabunge hao ni Faith Mtambo na Mary Chatanda (wote viti
maalumu (CCM), Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis
Kigwangala na Ali Mzee Ali ambaye
ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na mmoja wa Baraza la wawakilishi Zanzibar wameteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi ya
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).
Wabunge hao ni Faith Mtambo na Mary Chatanda (wote viti
maalumu (CCM), Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis
Kigwangala na Ali Mzee Ali ambaye
ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Katika orodha hiyo ya wajumbe wapya, pia yumo Wilson
Masilingi ambaye alikuwa Mbunge wa Muleba Kusini mpaka mwaka 2010, ambapo alishindwa katika
kura za maoni ndani ya chama chake na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Profesa
Anna Tibaijuka ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa inaeleza kuwa , Rais Jakaya Kikwete amemteua kwa
kipindi cha pili, Balozi Christopher Liundi kuwa mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa
kipindi cha miaka mitatu na kwamba uteuzi huo umeanza rasmi Machi 6,mwaka huu.
Liundi aliteuliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2010, huku
wajumbe wake wakati huo wakiwa ni Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro
Nyalandu, Rose Lugembe, Shabani Mnubi, Nuru Milao, Joseph Chilambo, Wilfred
Nyachia, Makumba Kimweri, Dk Aggrey Mlimuka na Issa Suleiman.
Wajumbe wengine wa bodi hiyo mpya ni Aggrey Mlimuka, Dash-Hood Mndeme, Dk Ali Mndali na Balozi mstaafu Abdi Mshangama.
No comments:
Post a Comment