Mwanachama wa CHADEMA akiwa amenyanyua kadi ya chama chake cha awali,na kukabidhiwa kadi ya CHAMA CHA MAPINDUZI
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Gairo,Mkoani Morogoro kwenye mkutano wake wa kumalizia ziara yake wilayani humo,katika uwanja wa Shule ya msingi Gairo jana jioni
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye akizungumza mbele ya wakazi wa Chakwale mara baada ya Shina la Kata hiyo kuzinduliwa mapema leo mchana,ndani ya wilaya ya Gairo.
Wazee wa Gairo wakimpa zawadi ya silaha za jadi Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana kabla ya kufanya mkutano wake wa hadhara jana jioni kwenye uwanja wa shule Msingi Gairo,Wilayani Gairo Mkoani Morogoro.
Ndugu Kinana akijaribu silaha ya jadi aliyokadbidhiwa na wazee wa Gairo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na wakazi wa Kata ya Chakwale,Wilaya ya Gairo mapema jana mchana,alipokuwa akizindua Shina jipya la Wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi CCM.Katika uzinduzi huo Kinana aliwaasa na kuwahimiza wakazi wa eneo hilo kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa kijitegemea badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu ikiwemo na suala la kuwapa ajira.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akiwapa kifuta jasho baadhi ya wazee-waasisi wa chama cha CCM,kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa shina jipya la kata yao ya Chakwale,Wilaya ya Gairo mapema leo mchana.Ndugu Kinana na Ujumbe wake wa CCM wako ndani ya Wilaya ya Gairo katika ziara ya kuimarisha chama cha CCM mkoani Morogoro sambamba na kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Baadhi ya Wazee waasisi ndani ya CCM-Kata ya Chakwale wakionesha kadi zao za chama cha CCM walizonazo tangu kuanzishwa kwa chama hicho,kwenye shughuli fupi ya kuzindua shina la kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Gairo,Mh.Shabiby akizungumza jambo na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye kwenye Kata ya Kibedya,Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro. |
No comments:
Post a Comment