
Mwanachama wa chama cha CHADEMA akikabidhi kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana,akiwa ni mwanachama mpya aliyejiunga na chama hicho.

Ndugu kinana akizindua moja shina la Wakaretwa wa chama cha CCM kati ya mashina manne aliyoyazindua Ifakara mjini.
Baadhi ya Wananchi wa eneo la Ifakara Mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana alipozungumza nao eneo la Stendi kuu ya mabasi ya Ifakara mjini,Ndugu Kinana alizungumza mambo mengi ikiwemo namna ya kufanya utatuzi wa mambo ambayo yamekuwa kero kwao,ikiwemo suala la Umeme,Kilimo na miundo mbinu,sambamba pia kuisaidia miradi mbalimbali inayofanywa na vijana wa mji wa Ifakara ambao unakuwa kwa kasi siku hadi siku.
Ndugu Kinana akikazia jambo wakati alipokuwa akizungumza na baadhi ya Wananchi wa eneo la Ifakara Mjini,eneo la Stendi kuu ya mabasi ya Ifakara mjini,wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanachama wa Ifakara mjini kwenye mkutano wao ndani.

Baadhi ya wanachama wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana alipozungumza nao kwenye mkutano wao ndani,Ifakara Mjini wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro,ambapo alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo na suala zima la kukiimarisha chama hicho.

Baadhi ya wakazi wa Ifakara Mjini eneo la Sokoni,wakimsikiliza Ndugu Kinana alipozungumza nao kwenye eneo la mradi wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment