Saturday, April 13, 2013

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI BARABARA YA TANGA-HOROHORO

JK ajivunia kasi ya ujenzi wa misingi ya uchumi


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC) na viongozi na wadau mbalimbali wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14. Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC)".
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14 akisaidiana na Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC), Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lenhardt, Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia baada ya kufungua rasmi barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14 akiwa na Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC), Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lenhardt.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kufungua barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14 akiwa ameongiozana na Naibu waziri wa wizara ya ujenzi, Mhe Gerson Lwenge (kulia), Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC), Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lenhardt, na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Chiku Gallawa (kushoto)

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti kama kumbukumbu ya ufunguzi rasmi barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14. Kushoto kwake ni Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC), na kulia kwake ni Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lenhardt, Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga.

Msafara wa Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ukipita juu ya sehemu ya barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14. Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC). Kukamilika kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.PICHA NA IKULU

KASI ya Serikali ya kujenga barabara kwa kiwango cha lami nchini imeendelea kuonekana, baada ya jana Rais Jakaya Kikwete kuzindua barabara mpya ya Tanga-Horohoro yenye urefu kilometa 65.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika eneo la Kasera makao makuu ya wilaya ya Mkinga, Rais Kikwete alisema hiyo ni ishara kuwa serikali imedhamiria kuboresha na kurahisisha maisha ya watanzania, hasa kwa kuzingatia kuwa barabara ndiyo kipaumbele namba moja katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya wananchi.

Pia ameahidi kuhakikisha anatengeneza mazingira mazuri ya kukamilisha utekelezaji wa mchakato wa uunganishaji wa barabara kuu za nchini zenye urefu wa zaidi ya kilometa 11,000 ambazo kwa asilimia 60 zinagharamiwa na serikali yenyewe kabla hajamaliza muda wake.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa mkoa wa Tanga kuacha malumbano ambayo yamekuwa yakichelewesha kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani mpaka Bagamoyo kwa kiwango cha lami ambapo mchakato wake umeanza .

Awali akimkaribisha Rais kuzungumza na wananchi, Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge alisema mpaka kukamilika kwa ujenzi wa Barabara ya Tanga/ Horohoro kumegharimu kiasi cha Sh bilioni 75.15, fedha ambazo zimetumika katika ujenzi wa madaraja saba, kumlipa mkandarasi, ulipaji wa fidia kwa wananchi waliojitolea kupisha ujenzi huo na ujenzi wa nyumba za ibada.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale alisema mchakato wa ujenzi wa barabara hiyo ulianza mwaka 2005 ambapo hatua mbalimbali za upembuzi yakinifu na kumpata mkandarasi na mhandisi mshauri zilifanyika.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardts na Mtendaji Mkuu wa MCC, Daniel Yohannes, walisema kuwa serikali ya watu wa Marekani inafarijika kuona serikali ya Tanzania imekamilisha yale yaliyokusudiwa katika suala zima la kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi.

Balozi Lenhardts alisema kuwa serikali ya watu wa Marekani imetenga zaidi ya dola milioni 698 kwa kupanua na kuboresha sekta za maji, barabara na umeme kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger