Serikali
yatangaza nafasi za kazi 1,134.
Serikali kupitia
Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia
Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi wazi za kazi kama zilivyo katika
Tangazo la Lugha ya Kiingereza na Kiswahili.
Kwa mujibu wa
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi
hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo
ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.
Daudi alifafanua
kuwa Waajiri hao ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wizaraya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa
Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu
Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara. Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Ofisi
ya Rais Maadili,
Wengine ni
Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga,
Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi,
Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha, Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la
Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga,Morogoro,
Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke.
Nafasi nyingine
ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Kyela, Rungwe, Mbeya,
Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete,
Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa, Meatu,
Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga,
Mpanda, Monduli, Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo,
Tabora, Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino,
Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa naTandahimba. Mkurugenzi Halmashauri ya Mji
Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA.
Katibu huyo
amesema kuwa nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika katika kada zifuatazo;
Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II – (Nafasi 10), Afisa Vipimo II –
Nafasi 6, Mpima Ardhi daraja la II (Nafasi 26), Mhandisi daraja la II – Ufundi
Umeme – Nafasi 9, Afisa Mipango Miji
daraja la II– Nafasi 13, Mhandisi daraja la II - Ujenzi (Nafasi 16), Mhandisi
daraja la II - Maji (Nafasi 13), Afisa
Misitu daraja la II (Nafasi 7), Afisa wa Sheria daraja la II – nafasi 3,
Mtakwimu Daraja la II – nafasi 8, Mthamini daraja la II – Nafasi 7, Mkadiriaji Ujenzi daraja la II – nafasi 4, Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II
– nafasi 1, Mhandisi Daraja la II – Nishati (Nafasi 3), Msanifu Majengo Daraja
la II– (nafasi 3) na Mjiolojia Daraja la II – Nafasi 7, Fundi Sanifu daraja la
II (Ujenzi) -Nafasi
26, Mvuvi
Msaidizi Daraja la II – nafasi 8 na Fundi Sanifu Msaidizi (Maji) -nafasi 19.
Nafasi nyingine
zilitotangazwa na Serikali ni Nahodha Daraja la II – Nafasi 6, Fundi Sanifu
daraja la II - Haidrolojia -Nafasi 6 ,Fundi Sanifu Daraja la II -Nafasi 6,
Msaidizi Misitu Daraja la II – nafasi 7, Fundi Sanifu Daraja II – Ramani –
Nafasi 6, Fundi Sanifu Daraja la II –Maendeleo ya Jamii– Nafasi 3, Dereva
Mitambo Daraja la II– nafasi 1, Mpiga
chapa msaidizi- Nafasi 5, Operata wa kompyuta msaidizi - nafasi 3, Fundi Sanifu
Daraja la II - Migodi – nafasi 9, Polisi Msaidizi– Nafasi 5, Mpokezi–Nafasi 1,
Katibu Mahsusi daraja la III-nafasi 10, Mlinzi –Nafasi 100, Dereva Daraja la II
– nafasi 178, Msaidizi wa Ofisi– Nafasi
30, Afisa Kumbukumbu daraja la II– nafasi 1,
Mwenyekiti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya – nafasi 5, Afisa
Mtendaji wa Kata Daraja la III– nafasi 10, Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la
II– nafasi 6.
Afisa Mtendaji wa Kijiji daraja la III) – nafasi 232, Afisa Mtendaji Mtaa daraja la III– nafasi 3, Afisa Lishe daraja la II– nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II - Ufundi
na Umeme, Afisa Biashara msaidizi–
Nafasi 1, Mchapa Hati daraja la II –
Nafasi 1, Mhandisi Daraja la II –Baharini-(nafasi 1), Dereva Mitambo Daraja la II – (nafasi 1), Dereva wa Vivuko daraja la II – Nafasi 3, Mkufunzi Mwandamizi Daraja II - Nafasi 1, Mkufunzi Daraja ii - Nafasi 2, Fundi
Sanifu Msaidizi (bomba)–nafasi 3, Fundi
Sanifu Msaidizi (Umeme) –Nafasi 4,
Mkufunzi Daraja II– nafasi 3, Mkufunzi
daraja la II -Jiolojia – nafasi 1, Mkufunzi
Msaidizi– Jiolojia – nafasi 1, Fundi
Sanifu daraja II -Ubunifu Mipango
Miji – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja
II- Urasimu Ramani – Nafasi 5, Fundi Sanifu daraja II- Uchapaji Ramani –Nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II -Maabara– nafasi 13, Fundi Sanifu Msaidizi (Ujenzi– nafasi
1), Fundi Sanifu daraja la II
-Nafasi 4, Wakufunzi wasaidizi –
nafasi 54 na Mhasibu Mkuu daraja II.
Katibu
alifafanua kuwa nafasi 949 zilizoko katika tangazo la Kiswahili ni kwa ajili ya
Waajiri walioainishwa hapo juu na kwa Tangazo la nafasi wazi 185 zilizoko
katika tangazo la lugha ya Kiingereza ni kwa ajili ya Taasisi na Wakala
mbalimbali za Serikali.
Daudi amesema
mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 9 Aprili, 2013.
Aidha, amewataka
waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo yote mawili ya kazi na
kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama yalivyo katika lugha ya Kiingereza
na Kiswahili kabla ya kutuma maombi yao.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya
Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Machi, 2013
No comments:
Post a Comment