Waziri Mkuu Mh. Pinda akimfariji mmoja wa majeruhi aliyekuwa amelazwa kwenye wadi katika Hospitali ya Mt. Meru |
Waziri Mkuu Mh. Pinda akiwa ameongozana na Mbunge wa viti Maalumu UVCCM (CCM) Mh. Catherine Magige wakiwafariji wagonjwa katika Hospitali ya Mount Meru. |
Waziri Mkuu akisaini daftari la maombolezo |
Majeneza 13 katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti cha
hospitali ya Mkoa Mt.Meru
|
|
Waziri Mkuu Mh. Pinda akifariji wafiwa
|
Mch. Kisiri Laizer akitoa neno la pole kwa wafiwa
|
Wafiwa wakiwa katika nyuso za huzuni ambapo wengine
walishindwa kuvumilia na kuangua vilio
|
Mstahiki Meya wa jiji Mh.Gaudence Lyimo akitoa salamu za
pole kwa wafiwa
|
Mh.Pinda akizungumza na kijana ambaye alinusurika katika tukio hilo ambaye hali yake inaendelea vizuri baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini |
Mkuu wa Mkoa Magessa Mulongo akitoa salamu za rambirambi kwa wafiwa |
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia hali halisi ya eneo la uchimbaji moramu katika Kata ya Moshono Mkoani Arusha akiwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama jana tarehe 2/4/2013 ambapo watu 13 walipoteza maisha papo hapo |
Kushoto - kulia : Naibu Waziri wa Madini,Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha (aliyejifunga mtandio) wakifuatilia kwa makini alichokuwa anaeleza Waziri Mkuu. |
Mabki ya mojawapo ya gari aina ya Scania lili;oangukiwa na kifusi cha moramu. |
Eneo la tukio. |
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele akiwa anaongea na wananchi katika eneo hilo |
Eneo la tukio baada ya kufanyiwa usafi. |
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitangaza kuyafunga rasmi machimbo ya moramu eneo la Moshono, Arusha hadi Serikali itakapoweka utaratibu mzuri wa shughuli mbalimbali za uchimbaji katika eneo hilo ili kuepusha maafa mengine
Hatua hiyo ya Pinda imetokana na ajali ya watu 13
waliopoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi juzi, wakati wengine wawili
walijeruhiwa kwenye ajali hiyo iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na mvua
zinazonyesha jijini Arusha.
Pinda alitoa agizo hilo alipotembelea eneo hilo pamoja na
kuwajulia hali majeruhi wawili waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mt Meru.
Majeruhi mmojawapo aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo baada
ya kuondoka Waziri Mkuu.
Baada ya kuwasili Arusha jana saa 7.30 mchana, Pinda
alikwenda moja kwa moja katika Hospitali ya Mt Meru kuwatembelea majeruhi hao.
Wakati wa ziara yake alishuhudia majeneza 13 yaliyokuwa na
miili ya watu waliofariki kwenye tukio hilo ambayo imehifadhiwa katika chumba
cha kuhifadhia maiti.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo Pinda alitoa
salamu za pole kwa waathirika kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete huku akilishukuru
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na wananchi waliojitokeza kuokoa maisha ya
watu katika tukio hilo. Alisema Serikali imeyafunga machimbo hayo, huku
akisisitiza kuwa Serikali kamwe haiwezi kuruhusu uchimbaji wa namna hiyo.
“Tutafunga kwa muda kama tulivyofanya Mugusu ili tujipange
vizuri na tupate nafasi ya kusaidiana, hatuwezi kuruhusu uchimbaji wa namna hii
halafu kesho na keshokutwa tukaonekana wapuuzi,” alisema Pinda.
Waziri Mkuu pia alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa
Mulongo kushirikiana na JWTZ kuimarisha ulinzi mkali katika eneo hilo ili watu
wasiweze kujipenyeza na kufanya uchimbaji nyakati za usiku.
“Mkuu wa Mkoa ashirikiane na jeshi kuimarisha ulinzi hapa
najua ni gharama kwa Serikali lakini ni nafuu kwetu pia,”alisisitiza Pinda.
MASELE ALONGA.......
Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele
aliwatupia lawama baadhi ya viongozi wa Serikali na Halmashauri ya Jiji la
Arusha kwa tabia ya kuendeleza kuchukua mapato katika uchimbaji wa eneo hilo
badala ya kuangalia usalama
Aliwataka viongozi wa jiji hilo kuacha tabia hiyo kwa kuwa
ikiendelea kuna uwezekano mkubwa wa kuwapoteza wapiga kura ambao ndiyo nguvu
kazi ya taifa
"Viongozi tukiendelea na tabia ya kupokea mapato bila kuangalia usalama wa watu
sehemu ya kazi ni kweli kuwa tutapoteza wapiga kura wetu"
Masele alisema kuwa wizara yake inaendelea kutoa kutoa
semina inayohusu uchimbaji katika mikoa yote Tanzania lengo ni kuwaelimisha
wachimbaji huku akidai kuwa ukosefu wa elimu inachangia wachimbaji wengi
kupoteza maisha
"Mfano eneo hili halifai kuchimba kwa kwenda chini kwa
sababu ni sehemu ya udongo haina miamba kwa hiyo nirahisi kuporomoka na
kufunika watu"alisema
Alitoa wito kwa wachimbaji kuzingatia usalama katika eneo la
kazi,kuzingatia sheria za uchimbaji,kupokea utaalamu kwa wataalamu
MKUU WA MKOA ARUSHA
Akitoa salamu za pole mbele ya Waziri mkuu pamoja na
viongozi wa dini,wananchi,wafiwa,viongozi mbalimbali Mkuu wa Mkoa Magessa
Mulongo alisema kuwa tukio hilo ni kubwa sana huku akitoa shukrani kwa
wananchi,vyombo mbalimbali vya dola kuwez kushirika katika zoezi la uokoaji
miili
"Tukio lilitokea tarehe 1/4/saa 4 asubuhi na zoezi la
uokoaji miili liliendelea hadi mida ya saa 12 jioni ambapo maiti 13 ziliokolewa
MEYA WA JIJI LA ARUSHA
Meya wa jiji hili Gaudence Lyimo alisema kuwa Taifa
limepoteza vijana chapa kazi ambao ni
nguvu kazi ya Taifa
Alisema uongozi wa jiji umeshiriki katika mchakato mzima wa
maandalizi ya mazishi huku akitoa pongezi kwa jamii kujitolea kushiriki katika
zoezi hilo lililokuwa gumu
KIONGOZI WA DINI
Mchungaji Kisiri Laizer wa kaninisa la kkkt dayosisi ya
kaskazini kati aliwataka wafiwa kuwa na moyo wa uvumilivu na kuendelea kumuomba
Mungu kwa kuwa yeye ndiye muweza wa yote
Hata hivyo wakati wa ziara hiyo viongozi mbalimbali waliweza
kujionea hali halisi ya eneo hilo ambapo kifusi kingine kilidondoka katika eneo
hilo mida ya saa 4 asbuhi ila haikuleta
madhara kwasababu hazikuwepo shughuli za uchimbaji
WALIOPOTEZA MAISHA MAJINA YAO
Nibart Raphael,Christipher L.Kawishe,Jerald Masai,Japheti
Nellyang,Gerald Nellyang,Japhet Raphael,Elibariki Loseriani,Fabian Bambo,Fredy
Loserian,Eliasi Fanuel,Alex Maliaki,Julius Peter Pallangyo,Gerald Jacob
No comments:
Post a Comment