Bandari ya Kismayo ikemuwa ikitumika tangu Al Shabaab kufurushwa |
Mkutano wa kikanda kuhusu uekezaji na ukarabati nchini Somalia umeanza hii leo, mjini Nairobi, Kenya.
Waandalizi wa mkutano huo, wanasema kuwa lengo la mkutano ni kuangazia nafasi za uekezaji nchini Somalia kwani nchi hiyo sasa imeanza kuonekana kuwa thabiti
Mkutano wenyewe unahudhuriwa na wanasiasa wa kikanda na wa kimataifa , wafanyabiashara na wataalamau wa maswala ya kiuchumi.
Mapema mwezi huu , wafadhili katika mkutano wa kimataifa wa wafadhili mjini London, waliahidi kuchangisha dola milioni miamoja na thelathini.
Waekaji wamezungumzia maswala ya usalama na changamoto nyinginezo ambazo zinaweza kuwakabili waekezaji walio na moyo wa kufanya biashara nchini Somalia.
Licha ya mazingira kuwa bora kuliko siku za nyuma, watu nchini Somalia wangali wanakumbwa na visa vya utobu wa usalama hasa katika mji mkuu Mogadishu.
Wanamgambo wa Al Shabaab walifurushwa kutoka mji huo kufuatia juhudi za majeshi ya Muungano wa Afrika kwa kusaidiana na jeshi la Kenya na Somalia kupambana dhidi ya wanagmbao hao.
Kwa sasa wangali wanadhibiti maeneo yaliyoko nje ya mji mkuu ambako hufanya mashambulizi ya kuvizia.
Licha ya changamoto hizi, kunao waekezaji wa Somalia ambao wamerejea nchini humo kutoka mfano Uingereza na Marekani kuja kufanya biashara. Maisha mjini Mogadishu pia yameweza kubadilika kwani mji huo una taa nyakati za usiku na maisha huendalea kama kawaida huku mikahwa na vilabu ikiwa wazi kwa wanaopenda maisha ya kujitumbuiza nyakati hizo.
No comments:
Post a Comment