Tuesday, May 28, 2013

MSANII MAARUFU NCHINI NGWEA AFARIKI DUNIA



MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Albert Mangwea 'Ngwea'au mimi au Cowboy amefariki dunia Afrika Kusini leo.

Taarifa zilizopatikana leo kutoka Afrika Kusini ambapo inasemekana msanii huyo alikuwa akiishi, zinasema Ngwea alifikwa na umauti mapema leo.

Habari toka afrika kusini zinasema kuwa Ngwea a.k.a mimi, Coboy alifikwa na umauti kwenye hospitali ya  St Hellen mjini hapo Johanesbaerg alikokuwa amelazwa.

Hata hivyo, haijajulikana mara moja sababu ya kifo cha Mangwea ambaye alikuwa mmoja wa wasanii kutoka  chamber squad 'East Zoo'.

Mangwea alianza kujulikana kwenye ulimwengu wa muziki mwanzoni mwa miaka ya 2000 na nyimbo zake zilizomtambulisha vilivyo na kujizolea mashabiki wa muziki ni Mikasi na  Gheto Langu.

Ngwea ameshirikiana na wasanii kaza wa Muziki wa Kizazi kipya hapa nchini kama AY, TID, Mchizi Mox, Ferouz, Raha P na wengine kibao.


No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger