Wednesday, May 29, 2013

CCM NJOMBE HAIKAMATIKI

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana afunika Njombe

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa CCM, kwenye Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, May 28, 2013. Kinana ambaye yupo katika ziara ya siku saba, kukagua utekelezaji wa ilani ya chama na kuzungumza na wananchi mkoani Njombe, amefuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.


Baadhi ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika 

Mei 28, 2013 katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoani Njombe.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe,  May 28, 2013. Kinana ambaye yupo katika ziara ya siku saba, kukagua utekelezaji wa ilani ya chama na kuzungumza na wananchi mkoani Njombe, amefuatana na Katiobu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Ludewa na Vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, uliofanyika  katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, Mei 28, 2013. 
Sehemu ya umati wa watu wakishangilia jambo wakati Nduhu Kinana alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe,  Mei 28, 2013.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikujombe akizungumza na wananchi  wa Ludewa na vitongoji vyake waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa CCM, katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoni Njombe, leo May 28, 2013.Mbunge huyo aliwaeleza wananchi kuwa kwa sasa jimbo lake limepata fedha kwa ajili ya kujenga minara mitatu ya mawasiliano kwa ajili ya kuepuka kero ya mawasiliano mkoani humo,aidha aliyataja maeneo hayo kuwa ni Lupingu,Makonde pamoja na Madope .Mh Deo aliongeza kufafanua suala la ujenzi wa barabara,alibainisha kuwa suala la ujenzi wa barabara unaendelea vizuri kwani tayari serikali imekwisha mtengea fedha kwa ajili ya ujenzi wa kilometa 10 za lami kwa ajili ya Wilaya ya Ludewa,akaongeza kuwa Serikali imemtengea kiasi cha fedha Bilioni 1.2 kwa ajili ya kutatua tatizo la maji kwa wananchi wa wilaya ya Ludewa. 
3Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa mjini Ludewa .
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa shina la CCM tawi la Itunda kata ya Malangali mapema leo,alipotembelea mashina kadhaa kwa kuzungumza nao mambo mbalimbali ya kuimarisha chama.
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  alipokuwa akihutubia katika kijiji cha Malangali .
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amembatana na ujumbe wake wakitembelea mashina ya chama hicho sambamba na kuzungumza na wanachama katika tawi la Itunda kata ya Malangali, kwa madhumuni ya kuyakagua mashina hayo na kuimarisha chama.
Baadhi ya Wanachama wapya wapatao 60 walijiunga na CCM katika kijiji cha Malangali,pichani baadhi yao wakila kiapo.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger