Friday, July 19, 2013

HAFLA FUPI YA KUMTAMBULISHA BALOZI MULAMULA KWA MABALOZI NA VIONGOZI WA JUMUIYA MBALIMBALI DMV

Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani umemfanyia hafla fupi ya kumtambulisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwa kwa Whe. Mabalozi wa nchi jirani na nchi marafiki wa Tanzania wakiwemo viongozi wa jumuiya mbalimbali za Watanzania DMV.

image
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula akiwa na Rais Barack Obama mara baada ya kuwasilisha hati ya utambulisho katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama White House jijini Washington DC 

Kaimu Balozi na Mkuu wa Utawala na Fedha Mama Lily Munanka (kati) akimkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula mara tu alipowasili Ubalozini hapo akiambatana na familia yake, kulia ni Charles Gray ambaye ni Balozi wa hiari anayeitangaza Tanzania nchini Marekani na anayeishi Pennsylvania kwenye mji uitwao Bala Cynwyd.
Photo by Michuzi

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Charles Gray.
Photo by Michuzi

Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa.
Photo by Michuzi

Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa.
Photo by Michuzi

Kaimu Balozi na Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka akiongea machache yakiwemo kuwakaribisha Whe. Mabalozi na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV kwenye Hafla hiyo fupi na baadae kumkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuongea nao.
Photo by Michuzi

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea machache yakiwemo kuwashukuru Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi kwa kuandaa Hafla hiyo fupi ya kumtambulisha kwa Whe. Mabalozi wa nchi jirani na nchi marafiki wa Tanzania na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV wakiwemo wanahabari wa DMV pia alielezea kwamba leo Alhamisi July 18, 2013 alipeleka hati yake ya utambulisho kwa Rais Barack Obama na anafuraha kukutana nao hapo Ubalozini na hii isiwe mwisho wanakaribishwa muda wote wajisikie wapo nyumbani.
Photo by Michuzi

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Afisa Mindi Kasiga ili aongoze kuimba wimbo wa Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote. Mindi Kasiga ndiye aliyekua mshereheshaji wa Hafla hiyo.
Photo by Michuzi

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akitambulisha familia yake kutoka kushoto ni mwanaeTanya, Alvin na Mumewe Bwn. George Mulamula.
Photo by Michuzi

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifanya tosi.
Photo by Michuzi

Whe. Mabalozi, Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV, wageni waalikwa wakitosi pamoja na Mhe. Balozi.
Photo by Michuzi
Balozi Mula mula alitoa shukrani za dhati kwa mabalozi wenzake waliofika kumpongeza pamoja na Mh.E.L Mbunge wa Monduli na Watanzania wote waliokuwapo kwa kuhudhuria hafla hiyo.

Pamoja na mambo mengine alieleza pia kushangazwa kwake na kufurahishwa na mapokezi yasiyo na makuu yalio ya kifamilia zaidi aliyopewa huko White house na Rais Barack Obama na familia yake alipowasilisha hati zake za utambulisho siku ya alhamisi Julai 18.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger