Thursday, July 25, 2013

KISUMO: MBOWE ACHA KUITUMBUKIZA NCHI YETU KWENYE UVUNJIFU WA AMANI.

Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo, amemvaa Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe akimtaka aache kile alichodai ni kuitumbukiza nchi kwenye machafuko.


Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo
Na Daniel Mjema

“Unaposema huna imani na JWTZ, huna imani na Polisi wetu unataka kuanzisha vikundi vya kukulinda tafsiri yake ni kwamba unataka kuanzisha vikundi vyenye sare hii si sahihi,” alisema.



Akizungumza na gazeti la Mwananchi jana, Kisumo alisema kauli ya Mbowe inamaanisha anataka kupata msaada wa vijana wake kufundishwa kumlinda yeye na kuhoji ni nchi gani inafadhili chokochoko hizo.

“Zipo nchi zina mapesa mengi na zipo tayari kufadhili machafuko nchi nyingine lakini nchi zilizostaarabika kama Ujerumani, Marekani, Uingereza na nyingine haziwezi kujiingiza huko,” alisema.



Alisema anaamini hata Ujerumani ambayo imekuwa ikikifadhili Chadema, haitakubali kutoa fedha kufadhili uanzishwaji wa vikundi hivyo vya ulinzi wakati vyombo halali vya ulinzi ni Polisi na JWTZ.

Kisumo alifafanua kuwa vyama vya siasa vina sare zake na kusema CCM, Chadema na Cuf navyo vina sare lakini kutaka kuanzisha vikundi vya ulinzi inamaanisha vitapaswa kuwa na sare za kijeshi.

Kwa mujibu wa Kisumo, anaamini vyombo vya ulinzi na usalama nchini havitaruhusu kutekelezwa kwa mpango huo kwani unalenga kuwachochea wafuasi wa Chadema kutokutii mamlaka ya dola.

Suala la Chadema kutangaza mpango wake wa kuanzisha vikundi vya ulinzi limeibua mjadala mkali kati yake na CCM ambacho kinamiliki kikundi cha Green Guard huku Chadema wakimiliki Red Brigade

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger