Friday, July 19, 2013

MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA ATETA NA SWAHILI TV JIJINI WASHINGTON DC

Mhe. Edward Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kamataifa

image



Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Edward Lowassa, amemsifia Rais Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshima katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.

Alisema kitendo cha Rais wa Marekani Bwana Barack Obama kuja nchini na viongozi mbalimbali wa mataifa makubwa kumeonyesha Rais Kikwete anakubalika.

“Ni hivi karibuni tu Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani George W.Bush walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa Lowassa.

Mheshimiwa Lowassa ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, aliongeza kwa kusema, Rais Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi zingine labda kama mko juu sana katika medani za kimataifa.

Pia alisema Rais Kikwete amekuwa akihusishwa na utatuzi au ushauri wa kutatua matatizo mbalimbali ya nchi zingine na pia ameanza kuishirikisha Tanzania katika usimamizi wa amani katika nchi mbalimbali.

Tanzania iliweka historia hivi karibuni kwa maraisi wawili wa Marekani kukutana katika nchi moja kwa wakati mmoja, Rais Barack Obama na George W.Bush walikutana jijini Dar es Salaam mwezi huu

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger