Friday, July 19, 2013

MH. PINDA ASHUHUDIA UPAKUAJI WA MABOMBA YA GESI BANDARI YA MTWARA

MABOMBA YA GESI YAWASILI BANDARI YA MTWARA

image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuzindua utelemshaji wa mabomba ya gesi kutoka kwenye meli kwenye bandari ya Mtwara Julai 18, 2013. Mabomba hayo yatatandikwa chini ya ardhi kusafisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam. Kulia kwake ni Balozi wa China nchini, Dr. Lu na Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini , Stephen Masela. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Balozi wa China nchini, Dr. Lu kabla ya kushuhudia upakuaji wa mabomba ya gesi kwenye bandari ya Mtwara , Julai 18, 2013. Mabomba hayo yatatandikwa ardhini ili kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam.
Picha n Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia (wa pili kushoto) wakati alipozindua uteremshaji wa mabomba ya gesi kutoka kwenye meli bandarini Mtwara, Julai 18, 2013. Mabomba hayo yatatandikwa ardhini ili kuwezesha usafirishaji wa gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam.
Picha n Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Hassan Kasuguru,nahodha aliyeingiza bandarini Mtwara meli yenye mabomba ya gesi kutoka China wakati alipozindua upakuaji wa mabomba hayo Julai 18, 2013.
Picha n Ofisi ya Waziri Mkuu.

No comments:

Post a Comment

 
Support : Katibu Mwenezi CCM (w) Arusha | Jasper Kishumbua | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali Blog - Arusha - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper Kishumbua
Proudly powered by Blogger