Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose
Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya
Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea maeneo hayo na
kuweza kujionea changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wananchi hao ikiwa
ni pamoja na kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la
Kimataifa litakalowanufaisha wakazi wengi wa wilaya hiyo ambao wako kando kando
ya Mto Maragarasi unaopakana na nchi jirani ya Burundi.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose
Migiro akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha
Mnanila,Wilayani Buhigwe.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose
Migiro (pili kulia) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli
Mbegesi Charles (kushoto) kuelekea kwenye eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi
unaotenganishwa na sehemu ya Mto Maragarasi.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose
Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mnanila kilichopo kwenye Wilaya Mpya
ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata
zote zilizopo wilayani humo.
No comments:
Post a Comment