Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi hii ya Februari 16, 2015
amekwenda kuhani na kufariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa
na watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani maeneo ya kijiji cha Kibiki,
Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani iliyotokea Februari 11, 2013 na kupoteza
hapohapo maisha ya watu nane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria
wanane kugongana uso kwa uso na roli la mizigo.
Familia alizokwenda kuhani na kuzifariji ni pamoja na za
marehemu Hassan Erasto Kurunge (57), Maria Sadiki ((52) na mtoto wa mwaka mmoja
Samweli Ismail wa kata ya Ubena.
Wengie ni marehemu Essau Enos Mwamgingo (16) , Stella Isaack
Kazimoto (18), Bahati George Mbena (17) na Latifa Maneno (17).
Akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Mwantumu
Mahiza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Ahmed Kipozi, Rais Kikwete alieleza
kusikitishwa kwake kwa ajali hiyo, na kuwataka madereva wawe makini katika
kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Rais Kikwete alisikitishwa zaidi kwa taarifa kwamba gari hilo dogo lilikuwa
limebeba abiria wanane, na kuwa dereva wake ambaye pia alipoteza maisha, hakuwa
makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole na
kuwafariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na
wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki,
Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu
wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo
aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso
na roli.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya picha za
ajali hiyo alizopewa na wanafamilia walioondokewa na watoto na wazazi wao
kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena
Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane
wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya
Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji ndugu, jamaa na
marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya
barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa
Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II
lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Haya ndio magari yaliyopata ajali hiyo na kupelekea vifo vya
watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze.PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment