Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Muasisi wa Chama, Mohammed Matipa alipowasili
Ofisi ya CCM, Tawi la Tulieni Kata ya Jamhuri Lindi mjini, leo Feb. 19, 2013.
Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiimba wimbo wa 'Wanawake na
Maendeleo', kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Tulieni, Kata ya Jamhuri Lindi mjini, leo Feb 19, 2013.
Wakereketwa wa CCM
Mwajabu Abdulrahman (kulia) na Saida Mtopa, wakishangilia wakati Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipokuwa
akihutyubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Tulieni, Kata ya Jamhuri,
Lindi mjini leo, Feb 19, 2013.
Wanachama wapya wa
CCM wakila kiapo baada ya kukabishiwa kadi zao na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Feb
19, 2013, kwenye Kijiji cha Tulieni Kata ya Jamhuri Lindi mjini.
Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Jamhuri Lindi mjini, wakimsikiliza Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (hayupo
pichani), alipozungumza nao katika kikao cha ndani, kwenye Ofisi ya CCM, tawi
la Tulieni katika Kata hiyo leo, Feb 19, 2013.
Bi, Fatuma Jaluo (78)
akifuatilia kwa makini msafara wa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ulipopita
karibu na nyumbani kwake, katika kijiji cha Tulieni, Kata ya Jamhuri wilaya ya
Lindi mjini leo, Feb 19, 2013.
Kina Mama wa CCM,
wakishiriki kula kiapo cha mwanachama wa CCM wakati wanachama wapya
waliokabishiwa kadi na Mama Salma Kikwete walipokuwa wakipa, kwenye mkutano
uliofanyika kijiji cha Tulieni, kata ya
Jamhuri wilaya ya Lindi mjini, leo Feb 19, 2013. Kutoka Kushoto ni Fatuma
Mohamed, Aswila Ditopile na Zitta Maliyaga ambaye ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa
Lindi.
Vijana 36 waliokuwa
wanachama wa CUF na kuamua kuhamia CCM, wakimsiliza mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akipohutubia mkutano wa hadhara jana, Feb 19, 2013, kwenye Kijiji cha
Mitandi, Kata ya Mbanja, Lindi mjini.
Baadhi ya waandishi wa habari, waliopo kwenye ziara ya Mama
Salma Kikwete mkoani Lindi, wakiwa wameketi kwenye mkeka wakati wa mkutano
uliofanyika kijiji cha Tulieni, Kata ya Jamhuri Lindi mjini leo Feb 19, 2013.
Kushoto ni Mwenyeji wa kijiji hicho, Khalfan Dimoso. (Picha zote na Bashir
Nkoromo).
No comments:
Post a Comment